Na Anna Nkinda – Maelezo, Lincoln
Taasisi
ya fursa ya Elimu (Opportunity Education) ya nchini Marekani imeazimia
kuanzisha mradi wa laptop ndogo (tablets computer) kuanzia mwezi
Januari mwaka 2014 nchini ambazo zitatumika kufundishia ili walimu
waweze kufundisha haraka na kwa ufanisi zaidi pia wanafunzi watapata
nafasi ya kujifunza zaidi.
Hayo
yamesemwa jana na Joe Ricketts ambaye ni mwanzilishi na mtendaji mkuu
wa taasisi hiyo wakati wa hafla ya kuchangia uugwaji mkono wa utoaji
elimu barani Afrika iliyoandaliwa na taasisi ya Malaika ya nchini humo
na kufanyika katika chuo Kikuu cha Nebraska kilichopo mjini Lincoln .
Ricketts
alisema mradi huo kwa mara ya kwanza utaanzia nchini Tanzania ambapo
wanafunzi zaidi ya 1000 kutoka shule 10 tofauti watapewa laptop ndogo
kwa ajili ya kusomea na baada ya kipindi cha mwaka mmoja watafanya
mtihani ili kuangalia tofauti iliyopo kwa wale waliokuwa wakitumia na
wasiotumia.
Baada
ya majaribio hayo kama kutakuwa na mafanikio basi mradi huo utasambazwa
katika shule nyingine nchini Tanzania ili kila mwanafunzi aweze kupata
nafasi ya kusoma kwa kutumia laptop hizo na hii itakuwa ni nafasi kwao
ya kuweza kujitunza zaidi.
“Kwa
mara ya kwanza nilipokuwa nchini Tanzania nilipita Serengeti na
kukuta mtu anajitahidi kutengeneza nyumba ambayo ni ngumu
kuitengeneza hii inamaana kuwa mwalimu mmoja alikuwa anafundisha
wanafunzi zaidi ya miamoja niliamua kuanzisha mahusiano na shule hiyo
ambayo niliwapelekea vifaa mbalimbali vya kufundishia”.
“Lengo
la kuanzishwa kwa Taasisi hii ni kutoa msaada wa kielimu ikiwa na nia
ya kufanya upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi kutoka nchi
zinazoendelea ili wale wanaotoka katika familia maskini waweze kusoma na
kupata ajira pale watakapokuwa wamemaliza masomo yao na hivyo
kujikwamua na hali ngumu ya maisha”, alisema Ricketts.
Alimalizia
kwa kusema kuwa program zao za kufundishia wanafunzi zimeandaliwa kwa
lugha ya kiingreza lakini hivi sasa wameanza kuandaa program hizo kwa
njia ya Kiswahili jambo ambalo litazifanya shule ambazo zinafundisha kwa
lugha hiyo nazo kunufaika na Taasisi hiyo.
Kwa
upande wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliishukuru taasisi hiyo kwa
kusaidia kuboresha elimu nchini na kuiomba kuangalia uwezekano wa
kuzifikia shule, walimu na wanafunzi waliopo vijijini ambao nao
wanahitaji kupata njenzo nzuri za kufundishia na material mazuri ya
kusoma kama ilivyo kwa wanafunzi wa mjini.
Mama
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeeo
(WAMA) alisema kuwa kupitia taasisi hiyo ameweza kuwasaidia watoto wa
kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi ambao
hawakupata nafasi ya kupata elimu kuwapatia ufadhili wa masomo na hivyo
kuendelea na masomo yao.
Pia
ameweza kuinua uchumi wa wanawake jambo ambalo limewafanya waweze
kuimarisha hali zao za maisha kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na
kuwaongezea mitaji ya vikundi vyao vya maendeleo.
Mama
Kikwete alisema, “Nakupongeza Bwana Ricketts kwa kazi unayoifanya ya
kuzisaidia shule zaidi ya 400 nchini Tanzania msaada unaoutoa wa vifaa
vya kufundishia unawafanya walimu waweze kufundisha masomo yao vizuri
naamini tutajenga mahusiano mazuri kati ya Taasisi yako na WAMA ili
kuhakikisha kuwa program hii inafanikiwa na kutimiza malengo yake”.
Taasisi
hiyo ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa nchini mwaka 2006 walianza
kufanya kazi na shule moja ya msingi na hadi kufikia sasa shule 434
zikiwemo za Sekondari 33 zimenufaika kwa kupata vitabu, DVD na zana za
kufundishia.
Kwa
upande wa shule za sekondari wanatoa mwongozo wa mwalimu ambao
unamuongoza kirahisi jinsi ya kuwafundisha wanafunzi , laptop ambazo
zinamasomo yaliyorekodiwa ambayo ni ya sayansi, hesabu, kiingereza na
maarifa ya jamii ,projecta na Televisheni ambazo zinasaidia kuonyesha
masomo na vitabu na video inawasaidia wanafunzi kujifunza somo la
kiingereza kwa njia ya kusikiliza na kusoma.
Mama
Kikwete alipata nafasi ya kutembelea makao makuu ya Taasisi hiyo
yaliyopo katika mji wa Omaha na kujionea nyenzo mbalimbali za
kufundishia vikiwemo vitabu na DVD zikiwa zimefungwa kwa ajili ya
kupelekwa katika nchi mbalimbali zinazoendelea za bara la Afrika na Asia
ikiwemo Tanzania.
0 comments:
Post a Comment