Afsa
Mtendaji Mkuu Mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Bi. Elena
Senkoro akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya cheti
cha makabidhiano ya nyumba 20 za watumishi wa idara ya afya zilizojengwa
Mkoani Rukwa na mfuko huo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi
wa jamii kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua
Kikuu na Malaria leo tarehe 28 Septemba 20113 katika kijiji cha
Chipu pembeni kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga. Anaeshuhudia katikati ni
Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt. Herman Lupogo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizindua rasmi moja ya nyumba
20 za watumishi wa idara ya afya katika kijiji cha Chipu baada ya
kukabidhiwa rasmi na taasisi ya Benjamin William Mkapa leo tarehe 28
Septemba 2013.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa katika picha ya pamoja
na mtumishi wa idara ya afya katika zahanati ya Chipu (kulia) ambaye
ataishi katika nyumba hii iliyojengwa na mfuko wa taasisi ya Benjamin
William Mkapa. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge Jimbo la Sumbawanga
Mjini Aeshi Hillal, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe na
Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Dkt.
Herman Lupogo
Moja ya nyumba 20 zilizojengwa na taasisi hiyo iliyopo Ntendo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Afisa
Mtendaji Mkuu Mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Bi. Elena
Senkoro akielezea miradi mbalimbali ya taasisi hiyo katika kusaidia
jamii ya watanzania.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitambulisha baadhi ya wageni katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akipanda mti wa kumbukumbu katika hafla hiyo ya makabidhiano.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipanda mti wa
kumbukumbu baada ya makabidhiano ya nyumba 20 zilizojengwa na mfuko wa
taasisi ya Benjamin William Mkapa Mkoani Rukwa.
Mbunge wa Jimbo la Sumbwanga Mjini CCM, Aeshi Hillal akipanda mti wa kumbukumbu.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akimnong’oneza jambo Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya muda mfupi baada ya
makabidhiano ya nyumba hizo.
Picha ya Pamoja.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Afsa Mtendaji Mkuu
wa Mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Bi. Elena Senkoro cheti
cha shukurani na kutambua mchango wao katika ujenzi wa nyumba 20 za
watumishi wa idara ya afya Mkoani Rukwa.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa)
0 comments:
Post a Comment