DIWANI ATHUMANI – ACP -KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
………………………………………………………………………..
“PRESS RELEASE” TAREHE 29. 09. 2013.
WILAYA YA MBARALI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO UTENGULE
WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. JIDAYI S/O JINGAZA, MSUKUMA, MIAKA
26, MKULIMA, NA MKAZI WA UTENGULE ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPATIWA
MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA IGURUSI BAADA YA KUJERUHIWA KWA KUPIGWA
NA FIMBO KICHWANI NA WATUHUMIWA WANNE AMBAO NI {1} DONGEA S/O INAMBILI
{2} KAMTIMBO S/O INAMBILI {3} INAMBILI S/O INAMBILI NA MTUHUMIWA MMOJA
AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA. CHANZO CHA MAUAJI NI UGOMVI ULITOKANA NA
WATUHUMIWA KUTAKA KUMBAKA DADA WA MAREHEMU, WATUHUMIWA WAMETOROKA MARA
BAADA YA TUKIO HILO JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO
WATUHUMIWA WALIYOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
|
|
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA SAA 20:45HRS HUKO
MASHALA IGURUSI BARABARA YA MBEYA/IRINGA. GARI NO T.274 AUA AINA YA
SUZUKI ESCUDO LIKIENDESHWA NA DEREVA JOHN S/O MSHONGO. MIAKA 38, MPARE
, DAKTARI, NA MKAZI WA FOREST MBEYA, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE
OBED S/O DONARD, MIAKA 32, MBENA, MKAZI WA MASHALA NA KUSABABISHA KIFO
CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU
KWA AJILI YA TARATIBU ZA MAZISHI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI,
DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA
VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBOZI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 28.09.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO
MLOWO BARABARA YA MLOWO/KAMSAMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI NO
T.372 BYD AINA YA T/NOAH LIKIENDESHWA NA DEREVA DAVID S/O ALEXANDER @
MWAIPUNGU, MIAKA 30, MNYAKYUSA, MKAZI WA MLOWO LILIMNGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU AITWAYE SHUKURANI S/O MBEMBELA, MIAKA 32, MNDALI, DEREVA WA
PIKIPIKI{BODABODA} NA MKAZI WA MLOWO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI
AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI VWAWA – MBOZI. CHANZO
CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KA
MISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment