Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ACP Diwani Athumani
………………………………………………………………………………………………..
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 27/09/2013 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KARUNGU – MAKONGOLOSI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA JOHN S/O MAKELELE, MFIPA, MIAKA 21, MKULIMA, MKAZI WA BWAWANI AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO 1 NA GRAM 500. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA NYARA ZASERIKALI.
MNAMO TAREHE 27/09/2013 MAJIRA YA SAA 04:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KISERU – LUALAJE WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA REGAN S/O MWANAHELA, MSAFWA, MIAKA 60, MKULIMA, MKAZI WA LUALAJE, AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI NYAMA YA MNYAMA MENDEJELE KIASI CHA KILO 3 NYUMBANI KWAKE. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU,TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOJIHUSISHA NA UWINDAJI HARAMU KWANI
NI KOSA LA JINAI NA ATAKAYEBAINIKA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA
DHIDI YAKE.
Signed by
{DIWANI ATHUMANI – ACP}
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment