“PRESS RELEASE” TAREHE 17. 09. 2013.
|
MNAMO
TAREHE 16.09.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISUTO
– MLOWO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. BOAZ S/O SAMSON,
MIAKA 25, MMALILA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ISUTO ALIUAWA KWA
KUCHOMWA KISU TUMBONI NA BAKEL S/O MSAFIRI. CHANZO KINACHUNGUZWA,
LAKINI UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA NI KUDHULUMIANA KATIKA MCHEZO WA
KAMARI KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI CHA ISUTO. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA
YA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
WILAYA YA MOMBA – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA KIFO.
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 16.09.2013 MAJIRA YA SAA 07:00HRS HUKO MPEMBA BARABARA YA
TUNDUMA /MBEYA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI CERNANI S/O SILUNGULE ,MIAKA
22, MNYAMWANGA, MKAZI WA MPEMBA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
CHANZO NI MWENDO KASI WA MWENDESHA GARI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA
MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA GARI AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE
MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
WILAYA YA MBARALI – KUPATIKANA NA SILAHA.
MNAMO
TAREHE 16.09.2013 MAJIRA YA SAA 00:10HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
KIBETE – MKUNYWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA SEBASTIAN S/O MARCUS,MIAKA 36, MHEHE, MKAZI WA IGOMA
WILAYA YA MUFINDI MKOA WA IRINGA AKIWA NA SILAHA MOJA BUNDUKI AINA YA
MARK IV NO. BX- 10400 NA RISASI MBILI BILA KIBALI. MBINU NI KUFICHA
SILAHA KATIKA MFUKO WA SANDARUSI NA KUPAKIA KATIKA BAISKELI. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUMILIKI SILAHA BILA KIBALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA
ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA
ISIVYO HALALI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO
TAREHE 16.09.2013 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA META JIJI
NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA SAIMON S/O
MLOTWA,MIAKA 26, MSAFWA, MKAZI WA ILEMI AKIWA NA BHANGI KETE SABA [07]
SAWA NA UZITO WA GRAM 35. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA
SURUALI YAKE. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[BARAKAEL N. MASAKI - ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment