Monday, September 2, 2013


Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wameibuka na ushindi mnono wa mabao 4-3 dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jijini Dar es salaam ukiwa maalumu kuwatambulisha wachezaji wapya watatu, Henry Joseph ambaye hakucheza leo kwani amejiunga na Taifa stars, Amissi Tambwe na Gilbert Kaze waliojiunga na Simba wakitokea Vital`o ya Burundi.
Katika mchezo wa leo, mshambuliaji mpya wa Simba Sc kutoka Burundi, Amissi Tambwe ameanza kazi katika klabu hiyo, baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-3 .
Mbali na kufamania nyavu mara mbilii, Tambwe pia alitoa pasi ya bao la pili- hivyo kuwapa imani kubwa Simba kuwa hawakukosea kumleta ligi kuu soka Tanzania bara.
Naye Mrundi mwenzake, Kaze aling`ara sana baada ya kusimama imara na kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika kipute hicho cha kukata na shoka.
Mafunzo ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Ally Juma na Simba walisawazisha dakika ya 45 kupitia kwa Tambwe.
demunga 1-001Jembe Jipya, Amis Tambwe limepiga mawili leo na kuwahakikishia Simba kuwa hawajafanya makosa kumsajili (Picha kwa hisani ya Sallehjembe.com)
simbaWazee wa Kidedea leo ilikuwa shangwe tu, limepigwa soka safi sana
Kipindi cha pili Simba waliingia kwa kasi na katika dakika ya 47, Sino Augostino aliiandika bao la pili klabu yake na dakika 5 baadaye Mafunzo walisawazisha bao hilo kupitia kwa Juma Jaku.
Kwa mara nyingine tena, Juma Jaku aliifungia Mafunzo bao la tatu katika dakika ya 72 na katika dakika ya 81, Nyota Tambwe alisawazisha bao hilo na kufanya ubao wa magoli usomeke 3-3.
Na Simba waliandika bao la nne na la ushindi katika dakika ya 83 kupitia kwa nahodha wake Masoud  Nassor “Cholo”  na kuwanyanyua mashabiki wa Simba Sc waliofurika kwa wingi kushuhudia mtanange huo.
Kikosi cha Simba SC:  Anderw Ntalla/Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Miraj Adam, Gilbert Kaze, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’/William Lucian ‘Gallas’, Ramadhani Singano ‘Messi’, Said Ndemla, Amisi Tambwe, Rashid Ismail/Sino Augustino na Ramadhani Chombo ‘Redondo’/Zahor Pazi.
Kikosi cha Mafunzo: Abdul Suleiman, Hamadi Hajji/Hajji Abdi, Abdul Abdallah, Heri Salum, Said Mussa, Juma Othman/Haji Mwambe, Mohamed Abdul, Masoud Hamad/Wahid Ibrahim, Juma Jaku, Ally Othman/Sadick Habib na Ally Juma.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video