Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
HATIMAYE
mzunguko wa nne wa ligi kuu soka Tanzania bara umeendelea kushika kasi
leo hii kwa timu zote 14 kushuka dimbani katika viwanja saba tofauti
nchini.
Wekundu
wa Msimbazi , Simba SC “Taifa Kubwa” chini ya kocha Abdallah Kibaden
`King Mputa` wamewakaribisha wapigwa kwata wa Mgambo Sooting Stars
wanaonolewa na kocha Ramadhan Kampira kutoka jijini Tanga `Waja leo
waondoka leo` katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudia
dakika 90 za kipute hicho zikimalizika kwa Mnyama kushinda mabao 6-0,
huku Mrundi Amis Tambwe akipiga manne peke yake.
Tambwe ambaye alipondwa hivi karibuni kwa kutofunga mabao aliandika mabao yake katika dakika ya 4, 42, 44, 88.
Kwa matokeo hayo, Mnyama amefikisha pointi 10 na kukaa kileleni mwa ligi hiyo.
Mabao
mengine ya Simba yamefungwa na Mtanzania kinda mwenye kasi kubwa na
ujuzi wa hali ya juu, Haroun Chonongo katika dakika ya 32 na 64.
Huko
jijini Mbeya `Jiji la kijani`, mabingwa wa ligi hiyo, klabu ya Yanga ya
Dar es salaam chini ya kocha Mhlolanzi, Ernie Brandts, kwa mara
nyingine tena wameshuka katika dimba la kumbukumbu ya Sokoine kuwakabili
maafande wa Tanzania Prisons `Wajelajela` na kushuhudia dakika tisini
zikimalizika kwa sare ya 1-1.
Bao
la kwanza la Yanga limefungwa katika dakika ya 41 kufuatia mpira mrefu
uliorushwa na Mbuyu Twite na kumkuta Simon Msuva ambaye alitoa pande
kwa Jerry John Tegete aliyezamisha mpira kimiani.
Prisons
walisawazisha bao hilo kupitia kwa Fredy Chudu katika dakika ya 77 na
kusababisha mabingwa Yanga kuvuna pointi 2 tu katika mechi mbili za
Mbeya na hatimaye kufikisha alama 6 kibindoni.
Nao Makamu bingwa wa ligi hiyo, matajiri wenye jeuri ya pesa, wana lambalamba, Azam fc wameoneshana
kazi na wageni wa ligi kuu wenye historia ya kupanda na kushuka,
Ashanti United `Watoto wa jiji` na kushuhudia dakika zote zikimalizika
kwa sare ya 1-1 na kumfanya kocha Sterwat John Hall azidi kupasuka
kichwa.
Dimba la CCM
Mkwakwani jijini Tanga limehimili daluga za wenyeji Coastal Union
`Wagosi wa Kaya” dhidi ya Rhino Rangers,ambapo mchezo huo umemalizika
kwa sare ya bao 1-1.
Kagera
Sugar walikuwa katika dimba lao la Kaitaba kuikabili JKT Oljoro na
kushuhudia vijana wa Jackson Mayanja aliyerithi mikoba ya Kibadeni
wakiwabamiza Oljoro mabao 2-1.
Mechi
nyingine ilikuwa huko dimba la Manungu Complex ambapo wana TamTam,
Mtibwa Sugar wamewakaribisha Mbeya City chini ya kocha Juma Mwambusi na
dakika tisini zimemalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
(0-0).
Mchezo
huo ulikuwa wa kwanza kwa Mbeya City kucheza nje ya uwanja wa nyumbani,
hivyo ni matokeo mazuri kwao kwani pointi moja si haba ugenini.
Huko
Uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani, wanandugu wawili, Ruvu
Shooting wamewakaribisha JKT Ruvu na kushuhudia soka la upinzani mkubwa,
lakini dakika zote zimemalizika kwa matokeo ya Charles Mkwasa na kikosi
chake kuwafumua JKT Ruvu kwa bao 1-0 na hivyo kushushwa rasmi kileleni
ambapo sasa Simba wameanza kubarizi baada ya kushusha mvua katika mchezo
wa leo dhidi ya Mgambo.
0 comments:
Post a Comment