Na Baraka Mpenja, Mbeya
Ligi
kuu soka Tanzania bara inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mechi tatu
kupigwa ambapo mechi inayowavutia mashabiki wengi wa kabumbu ni baina ya
vinara wa ligi hiyo, Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc dhidi ya wenyeji wao
katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam jioni ya leo, Maafande wa
JKT Ruvu.
JKT
Ruvu wataingia uwanjani wakiwa tayari wameporomoshwa hadi nafasi ya nne
wakiwa na pointi 9 na katika nafasi ya tatu baaada ya matokeo ya jana
Uwanja wa Sokoine, Coastal Union “Wagosi wa Kaya” wanakalia kwa pointi
10 wakitokea nafasi ya tano, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Kagera
Sugar waliofikisha pointi 11 sawa na Simba lakini wanatofautiana kwa
wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Wataweza
leo?: Mechi iliyopita Simba walitulizwa kwa sare ya 2-2 na Mbeya City
na pichani ndivyo walitoka Uwanjani Vichwa chini, na leo hii watakula
sahani moja na JKT Ruvu, je, Amis Tambwe kuendeleza ufundi wa kufumania
nyavu?
Mechi
hii ina mvuto wa aina yake kutokana na watani wa jadi wa Simba, klabu
Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting jana ukiwa ni
ushindi wa kwanza katik mechi tano walizoshuka dimbani.
Kwa
kawaida matokeo ya wanajangwani yataongeza ladha ya mchezo wa leo kwani
Simba watahitaji kushinda ili kuendelea kukalia usukani wa ligi hiyo na
kuwafanya Yanga wazidi kuisoma namba Kibadeni..
Pia
kuwa fiti wa Warundi, Gilbert Kaze na Amisi Tambwe kumeongeza hamu ya
mashabiki kuwaona wanandinga hao wakiendelea kung`ara, hususani Tambwe
ambaye anaoongozwa kwa kupachika mabao mpaka sasa akiwa nayo 6 katika
mechi mbili tu.
Nyomi yote hii iko nyuma ya Simba sc
Aidha
katika mechi hiyo, makocha wazalendo wanakutana kuanzia makocha wakuu
hadi wasaidizi, Abdallah Athuman Seif “King Kibadeni” na Jamhuri Kiwhelo
`Julio` kwa Simba, huku JKT Ruvu ikiongozwa na Mbwana Makata pamoja na
Greyson Haule.
Maarifa
ya wabongo hawa yatapimana leo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na
endapo Simba watashinda leo, watajikita zaidi kileleni wakifikisha
pointi 14 na kama Ruvu Watashinda watapanda juu zaidi kwa kujikusanyia
pointi 12 kileleni, lakini itategemeana kwani Azam wakishinda pia
watafikisha pointi 12 na hapo hesabu ya mabao itatumika.
Majembe: Azam FC nao wanasubiri balaa lao kutoka kwa Prisons leo
Uwanja
wa Sokoine kwa siku ya pili mfululizo utahimili daluga za Maafande wa
jeshi la Magereza Tanzania, Prisons ya Mbeya dhidi ya wana Lambalamba wa
Azam fc kutoka jijini Dar es salaam.
Tayaru
timu zote zimeshatambiana kuelekea mtanange huo ambapo katibu mkuu wa
Prisons, Inspekta, Sadick Jumbe ametamba kuwa klabu yake imejiandaa
vizuri kuvuna mtaji wa pointi tatu na vijana wake wako katika morali
kubwa.
Wakati
kwa upande wa Azam fc kupitia kwa Afisa habari wake, Jafar Idd Maganga
wamekiri ugumu wa mechi ya leo, hasa kutokana na ukomavu wa wapinzani
wao, lakini nia yao ni kushinda na kuchukua pointi tatu muhimu.
Mtawapigisha kwata Azam?: Prisons wana kibarua kizito leo uwanja wao wa sokoine jijini Mbeya
Mbali
na kipute hicho, vibonde wa ligi hiyo na uchochoro wa kuchukulia
pointi Msimu huu, klabu ya Ashanti United inaikaribisha Mtibwa Sugar
katika uwanja wa nyumbani wa Azam Complex, mbande Chamazi, nje kidogo ya
jijini la Dar es salaam.
Kama
waburuza mkia hao watashinda leo, halafu Prisons akafungwa, wajelajela
wataisoma namba mkiani, lakini kama Ashanti watashinda na na Prisons
wakishinda, wataendelea kuburuza mkia.
Kwasasa
Ashanti wanavuta mkia wakiwa na pointi moja tu katika mechi 6
walizocheza. Wamefungwa tano na kutoa sare moja na Azam fc.
0 comments:
Post a Comment