Wednesday, September 11, 2013


P2150200Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kukabidhi nyumba kwa wanachama 38, Mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA) unatoa shukurani kwa viongozi wa kijiji cha Mwanzega Kata ya Mbezi, Tarafa ya Shungubweni,wanavijiji pamoja na viongozi wa wilaya ya Mkuranga akiwepo Mkuu wa wilaya, Mercy Silla kwa kufanisha sherehe ya ugawaji nyumba na vyeti.
Wanachama zaidi ya 70 wamejitokeza kuchangia ujenzi wa nyumba ili wakabidhiwe Desemba 28, 2013 katika sherehe nyingine ya kukabidhi nyumba ambayo inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ambao waliomba udhuru sherehe ya awali.
SHIWATA inawahimiza wanachama wake wasifanye mzaha na kudharau mpango wa kuchangia ujenzi kwani utawanufaish na kuwamilikisha nyumba zao wenyewe kwa gharama nafuu.
Mtandao wa wasanii unatoa bure viwanja baada ya mwanachama kulipa gharama zote za kujiunga uanachama ambaye ataruhusiwa kujenga mwenyewe au kuchangia ujenzi wa nyumba kwa pamoja.
SHIWATA  inakusudia kujenga Shule ya Msingi, Sekondari na vyuo vya fani za utamaduni, Uandishi wa Habari na michezo mbalimbali ikiwemo soka kwa malengo ya kupata wachezaji bora ambao watanyanyua viwango vya michezo hiyo ndani na nje ya nchi ili kuwapatia vipato zaidi.
Pia inawahitaji wasanii, wanamichezo, wanahabari wenye vipaji na elimu ya juu katika fani zao wajiunge na SHIWATA ili waweze kuwa walimu wa sanaa na michezo mbalimbali ambayo itaanza kufundishwa kutoka ngazi ya Shule ya Msingi, Sekondari hadi Chuo katika kijiji cha Mwanzega.
Shule ya msingi itakapoanzishwa itatoa kipaumbele kwa masomo ya sanaa na michezo ili kupata wasanii na wanamichezo bora katika taifa letu.
SHIWATA pia inatarajia kujenga viwanja vya michezo, kumbi za Maonesho na Studio za kurekodia muziki na filamu zenye ubora ambazo zitauzwa ndani na nje ya nchi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video