Wednesday, September 25, 2013

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkaribisha Bondia Mstaafu Rashid Matumla (kulia) leo alipowasili ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 2- Sante (kilia) na Mtum(wakiongea) 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo(WHVUM) Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea na Bondia Mstaafu Rashid Matumla (Snakeman) alipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. 4- NKM(kulia) akiongea- (kat) Mtumla na (shot) MK  MIChe LEONARD THADEO 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo , Prof. Elisnate Ole Gabriel, (kulia) akiongea na  Bondia Mstaafu Rashid Matumla(wenye fulana ya mistari) leo jijini Dar es Salaam, ambapo ametakiwa kurithisha  kipaji chake kwa vijana nchini (kushoto) ni Mkurugenzi wa Michezo katika wizara hiyo Leonard Thadeo. 7-thadeo(SHT), matu (mist) na Elisant (kulia) 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) pamoja na Bondia Mstaafu Rashid Matumla (mwenye fulana ya mistari ) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara hiyo Leonard Thadeo(kushoto) wakati akitoa maelezo leo jijini Dar es Salaam , 11-group 
Picha ya pamoja – Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye miwani)  Mkurugenzi wa Michezo katika wizara hiyo  Leonard Thadeo( mwenye koti jeusi kulia), Bondia Mstaafu Rashid Matumla (mwenye fulana ya mistari)), pamoja na Afisa Vijana katika wizara , Amina Sanga(kushoto).
Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Na Concilia Niyibitanga
Wizara ya Hbari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemtaka Bw. Rashid Matumla ambaye ni bondia mstaafu katika mchezo wa ngumi za ridhaa kurithisha kipaji chake kwa vijana wengine.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel wakati akiongea na Bw. Matumla alipomtembelea ofisi kwake.
Prof. Gabriel amemtaka kuanzisha kikundi cha vijana ambacho ataweza kukifundisha mchezo huo ili kipaji chake kisipotee ukizingatia kuwa Tanzania ina wachezaji wachache katika mchezo huo.
“Ni vema ukarithisha ujuzi wako katika mchezo wa ngumi kwa vijana chipukizi kwa kuwafundisha na kuwashauri katika mchezo huo” Amesema Prof. Gabriel.
Amesema kuwa Serikali inatambua mchango wake katika mchezo wa ngumi hapa nchini na hivyo si vema akakaa na ujuzi wake ukizingatia kuwa yeye amestaafu katika mchezo huo.
Aidha, Prof. Gabriel ameongeza kuwa kwa kufanya hivo Matumla atawasaidia vijana chipukizi kuwa Mabondia wazuri wa baade ikiwa ni pamoja na kujiajiri badala ya kujihusisha na vitendo vibaya kama matumizi ya madawa ya kulevya n.k
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw. Leonard Thadeo amesema kuwa kikundi hicho kinaweza pia kikajihusisha na ujasiriamali kwa kuomba mikopo katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa kuwa wanamichezo pia wanatakiwa kujishughulisha na ujasiriamali ili kujiongezea kipato.
Kwa upande wake Bw. Matumla amesema kuwa amefurahi na amefarijika sana kuongea na viongozi wa wizara inayosimamia michezo na vijana kwa kuwa wameonesha kutambua mchango alioliletea Taifa hili katika mchezo huo.
Matumla amesema kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa anawarithisha mabondia chipukizi na vijana wengine kipaji chake katika mchezo huo ili wawe mabondia bora wa baadaye.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video