NA MAGRETH KINABO- MAELEZO
SERIKALI
ina mpango wa kuanzisha benki ya vijana amabyo itakuwa ikiwapatia
mikopo nafuu ili kuwawezesha kujiajiri wenyewe ikiwa ni hatua ya
kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa nchi.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif
Ali Iddi wakati wa uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu na
jinsi kwenye sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 uliofanyika katika
ukumbi wa Mwalimu Nyerere ,jijini Dares Salaam.
Makamu
huyo wa Rais alisema hayo kufutia chapisho hilo kuonesha kwamba
kundi la vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi miaka 35 kuwa ni
watu milioni 15.6 sawa na asiliamia 34.7 ya watu wote nchini.
“
Idadi hii ya vijana ikitumiwa vizuri itaongeza uzalishaji na hatimaye
kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umasikini ,” alisema Balozi Seif.
Aliongeza
kuwa Serikali na watu wengine wataendelea kuifanya Sera ya Maendeleo
ya Vijana ya mwaka 2007, ikiwemo kuhamasisha vijana kujiunga na
vikundi vya uzalishaji mali ni mojawapo ya mikkati ya kuendeleza vijana.
“
Kwa kuzingatia rasilimali zilizopo Serikali ina dhamira ya Kuimarisha
viwanda na Kilimo Kwanza kama njia nyingine za kuwazesha vijana kupata
ajira na kuongeza kipato. Vijana wa tabia ya kungojea ajira kazi za
maofisi ambazo haziko nyingi, bali wajiunge na kushiriki katika shughuli
za uzalishaji mali ili waweze kujaipatia kipato kwa ajili ya kuendesha
maisha yao,” alisisitiza.
Aidha
aliongeza kwamba kupitia chapisho hilo, limeonesha kuwa kundi jingine
la wazee wenye umri wa miaka 60 au zaidi amabo ni milioni 2.5 sawa na
asilimia 5.6 ya watu wwote nchini. Hivyo kulingana na Sera ya Wazee
kundi hilo linahitaji huduma maalum kama vile, matibabu, malazi na
huduma nyingine muhimu.
“Serikali na wadau wengine wataendelea kuwapatia wazee hawa huduma muhimu kulingana na hali ya uchumi wan chi,” alisema.
Balozi
Seif alizita Wizara ,Idara na Taasisi zote za Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuboresha
sera zilizopo na kutumia takwimu hizi katika kupanga mipango ya
maendeleo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) Dk.
Albina Chuwa alisema chapisho hilo linaonesha kuwa umri unaoanzia
miaka 0 hadi 4 kuashiria kuwa kiwango cha uzazi bado ni kikubwa.
Alifafanua
kuwa kwa kumujibu wa Utafiti wa Mama na Mtoto wa mwaka 2010 kiwango
cha uzazi ni wastani wa watoto 5.4 kwa kila mama mwenye umri wa miaka
15hadi 49, hivyo uzazi wa mpango utaendelea kusisitizwa.
Naye
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
(UNFPA)Mariam Khan alisema chapisho hilo litasaidia kujua iddai ya watu
wanaojiandikisha shule, wastaafu, kupanga uzazi wa mpango na mipango
mingineyo.
0 comments:
Post a Comment