PAMOJA na kumkosa mchezaji ghali
duniani, Gareth Bale, lakini mchezaji anayeliwa mshahara mkubwa zaidi
duniani, Cristiano Ronaldo alitosha kuipa pointi tatu Real Madrid usiku
huu, baada ya kufunga mabao yote katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Elche.
Bale atarejea katika mechi ya nyumbani
na Atletico Madrid Jumamosi wakati leo Ronaldo, ameendelea kuiweka Real
karibu vinara wa La Liga.
Ronaldo alifunga mabnao hayo katika
dakika za 51 na dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kutimu
dakika 90, wakati bao la kufutia machozi la Elche lilifungwa na Richmond
Boakye dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimua dakika 90.
Kikosi cha Elche kilikuwa: Elche: Manu
Herrera; Damián, Botía, Lombán, Albácar; Rubén Pérez, Carlos Sánchez;
Stevanovic, Coro, Fidel na Boakye.
Real Madrid: Diego López, Pepe, Ramos, Coentrão, Khedira, Ronaldo, Benzema, Arbeloa, Modric, Di María na Isco.
Raha: Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Madrid bao la pili
Moja zaidi: Cristiano Ronaldo akishangilia na wachezaji wenzake
Weka kule: Real Madrid ilicheza bila mchezaji ghali duniani, Gareth Bale
Beki wa Elche, Botia (kushoto) akikabiliana na mshambuliaji Mfaransa wa Real Madrid, Karim Benzema
0 comments:
Post a Comment