MCHEZAJI GHALI zaidi Duniani Gareth
Bale alisubiri mpaka saa moja iishe ndio aingie kwa mara ya kwanza
kuitumikia klabu yake ya Real Madridi katika michuano ya ligi ya
mabingwa barani Ulaya na kutoa mchango wake katika ushindi wa mabao 6-1
dhidi ya Galatasaray mjini Istanbul Uturuki, huku mchezaji anayelipwa
zaidi duniani kwa sasa, Cristiano Ronaldo akipiga matatu.
Bale alishuhudia wachezaji wenzake, Ronaldo, Isco, Benzema wakikipiga mabao kabla ya kuingia dimbani dakika 26 za mwisho.
Baada
ya kuingia Bale kwanza alitoa pande murua kwa Ronaldo kupitia mpira wa
adhabu na Mreno kukwamisha gozi kimiani kuandika bao la nne.
Halafu
alimpigia pande maridadi Ronaldo, ambaye alimmegea Benzema na
mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao lake la pili katika mchezo
huo.
Mabao
ya Real Madridi yalifungwa na Isco dakika ya 33, Karim Benzema 54 na 81
Mreno Christiano Ronaldo katika dakika za 63, 66 na 90, wakati bao la
kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Bulut dakika ya 84.
Mchezaji
bora wa mechi: Cristiano Ronaldo akiwa ameweka mpira wake ndani ya jezi
baada ya kufungwa hat-trick katika mchezo wa jana mjini Istanbul
Kazi nzuri: Cristiano Ronaldo akikumbatiana na Gareth Bale baada ya kufungwa bao lake la pili
Mchezaji ghali wa dunia alianzia benchi: Bale alitokea benchi na kuisaidia Real Madrid kushinda kwa kishindo
Wachezaji ghali wawili: Gareth Bale (kulia) akitembea pamoja na Cristiano Ronaldo baada ya kushangilia bao la pili
Kikosi
cha Real Madrid: Casillas (Lopez 14), Carvajal, Ramos, Pepe, Arbeloa,
Modric (Illarramendi 72), Khedira, Di Maria, Isco (Bale 64), Ronaldo,
Benzema
Wachezaji wa Akiba: Casemiro, Nacho, Jese, Morata
Mabao: Isco 33, Benzema 54, 81 Ronaldo 63, 66, 90
Aliyepata kadi: Pepe
Kikosi
cha Galatasaray: Muslera, Eboue, Chedjou, Nounkeu, Riera, Inan, Melo,
Baytar (Bruma 62), Yilmaz, Sneijder, Drogba (Amrabat 46)
Wachezaji wa Akiba: Iscan, Bulut, Balta, Kaya, Sarioglu
Bao: Bulut 84
Kadi: Melo, Amrabat, Riera
CHANZO: SPORTSMAIL
MATOKEO YA MECHI NYINGINE
|
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|
0 comments:
Post a Comment