Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
HALI
tete imezidi kutanda kwa kocha wa Manchester United, David Moyes baada
ya mshambuliaji wake chaguo la kwanza, Robin van Persie kutokuwa fiti
kuingia katika kipute cha kesho jioni dhidi ya majogoo wa jiji, klabu ya
Liverpool, kombe la Capital One nchini England katika dimba la Old
Trafford.
Imefahamika kuwa RVP atakuwa fiti katika mchezo wa mwishoni mwa wiki hii wa ligi kuu dhidi ya West Brom.
Mholanzi
huyo anayeibeba United katika safu ya ushambuliaji kwa sasa alipata
majeruhi ambayo yalimweka nje ya uwanja katika mechi ya watani wa jadi
dhidi ya mahasimu wao Manchester City dimba la Etihad na alikaa jukwani
kushuhudia mashetani wekundu wakinyanyaswa kwa kipigo cha mbwa mwizi
cha mabao 4-1, na wiki hii hajafanya kabisa mazoezi.
RVP
alipigwa picha akitoka katika duka la dawa , Alderley Edge akiwa
ameshika kiboksi cha dawa na hakwenda kabisa katika uwanja wao wa
mazoezi wa Carrington.
Huyuko
tayari: Robin van Persie hajafanya mazoezi na Manchester United wiki
hii na hatacheza kesho dhidi ya Liverpool, lakini alipigwa picha jana
akiwa na dawa
Anataka
kupoza maumivu: David Moyes anawataka wachezaji wake kuonesha kiwango
cha juu dhidi ya Liverpool, Capital One Cup, baada ya kula kipigo cha
mbwa mwizi wa dagaa kutoka kwa Manchester City cha mabao 4-1 jumapili
Akizungumzia
mechi Moyes amesema: ‘Sidhani kama Robin atacheza dhidi ya Liverpool.
Atakuwa na nafasi nzuri ya kucheza siku ya jumamosi”.
Akirejea
kipigo cha Etihad jumapili kuelekea mchezi dhidi ya Liverpool, Moyes
alisema: “Imepita. Siwezi kufanya chochote juu ya hili. Ilinishitua
sana, lakini ukiwa kocha wa muda mrefu kama mimi unatakiwa kushituka na
kujipanga”.
Hali tete: Moyes amesema kiwango cha City kimemshitua sana, lakini ni wakati wa kufikiria mchezo wa kesho dhidi ya Liverpool
0 comments:
Post a Comment