WASHIRIKI wa shindano la Redd’s Miss Tanzania leo watapata fursa ya kumjua mrembo wa kwanza kuingia katika hatua ya Nusu fainali ya Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati mrembo mmoja kati ya wanyange hao 30
atakapotajwa mshindi wa Miss Photogenic 2013.
atakapotajwa mshindi wa Miss Photogenic 2013.
Shindano hilo no moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusufainali ya shindano hilo litakalo fanyika baadae mwezi ujao.
Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.
Akizungumza na Father Kidevu Blog hii leo, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Uncle’ amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wanahabari wazoefu wa
masuala ya urembo Tanzania watakaa na kuchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.
masuala ya urembo Tanzania watakaa na kuchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.
Mshindi anataraji kutangazwa leo jioni katika hoteli ya Giraffe Ocean View na kujipatia tiketi hiyo.
Taji la Redd’s Miss Tanania Photogenic linashikiliwa na Mrembo Lucy Stephano aliyelitwaa mwaka 2012. Wafuatao ndio warembo watakao wania taji hilo hii leo.
Wafuatao katika picha chini ni baadhi ya warimbwende hao
0 comments:
Post a Comment