Thursday, September 12, 2013


1 (2) 
Na Renatus Masuguliko
Rais Jakaya Kikwete, amemwagiza Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, kuhakikisha kwamba ifikapo Oktoba, mwakani kero sugu ya maji wilayani Sengerema imepatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Aidha, amemtaka Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kusimamia utekelezaji wa ahadi ya Rais ya ujenzi wa barabara kiwango cha lami kutoka Sengerema hadi Kamanga yenye urefu wa kilomita 35 unakamilika kabla ya kumaliza muda wake.
Rais Kikwete alitoa maagizo hayo kwa staili ya kuwapandisha mawaziri majukwaani kubeba `misalaba’ yao wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa jana.
Agizo la Rais Kikwete lilifuatia taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, kuhusu kero sugu ya maji katika mji wa Sengerema.
Kero nyingine alizitaja kuwa ni ubovu wa barabara ya Sengerema hadi Kamanga, upungufu wa walimu,  miundombinu mashuleni na ukamilishwaji wa mradi wa umeme vijijini.
Rais Kikwete alisema Wilaya ya Sengerema  imetengewa  zaidi ya Sh. bilioni 1.3 kwa ajili ya uboreshaji huduma ya usambazaji maji kutoka chanzo cha Nyamazugo katika Ziwa Victoria hadi Sengerema.
Alisema mradi huo utatetekelezwa sambamba na mradi wa muda mrefu unaotekelezwa kupitia mradi wa uhifadhi mazingira wa Ziwa Victoria utakaogharimu Sh. bilioni 23.
Profesa Maghembe alithibitisha mji wa Sengerema kukabiliwa na uhaba wa maji ambapo alisema kwa sasa unapata lita milioni 2.3 za maji kwa siku badala ya mahitaji halisi ya lita milioni 7.8.
Kwa upande wake, Dk. Magufuli alisema mchakato wa kujengwa kwa barabara la Kamanga hadi Sengerema kwa kiwango cha lami ulikuwa mbioni kukamilika na kuwa utekelezaji wake ungeanza mara baada ya taratibu kukamilika.
Naye Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema vijiji 74 vitawekewa umeme   wilayani humo kupitia mradi unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani.
Hata hivyo, Profesa Muhongo aliwataka wananachi wawe tayari kulipia kwa kuwa hata wenye nyumba za zilizoezekwa kwa nyasi watawekewa umeme.
Rais Kikwete alikuwa katika ziara ya kikazi ya siku saba mkoani Mwanza.
CHANZO: GAZETI LA NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video