Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi ofisi ya ubalozi
wa heshima(Honorary Consulate) wa Tanzania jijini San Francisco nchini
Marekani leo jioni.Kulia ni Balozi wa heshima wa Tanzania jijini San
Francisco Mh.Ahmed Issa na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani
Mh.Liberata Mulamula na wapili kushoto ni Mke wa Balozi Mama Sherry
Julin Issa.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Heshima wa Tanzania jijini San FranciscoMh.Ahmed Issa,(wapili kushoto)
muda mfupi baada ya kufungua ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini San
Francisco nchini Marekani leo jioni.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini
Marekani Mh.Liberata Mulamula na kulia ni mke wa balozi Ahmed Mama
Sherry julin Issa.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio
jijini San Francisco Marekani muda mfupi baadaya kufungua ubalozi wa
heshima wa Tanzania na kuzungumza nao leo jioni.
Rais
Dkt.Jakaya MrishoKikwete akizungumza na baadhi ya Watanzania waishio
jijini San Francisco Marekani leo jioni.Rais Kikwete yupo nchini
Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atahutubia
kikao cha 68 cha Umoja wa Mataifa Jijini New York Marekani(picha na
Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment