Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya push Push Media Mobile Rugambo Rodney.
….
Mwandishi Wetu
Kampuni
ya Push Mobile Media itatoa zawadi ya gari aina ya vits kwa mshindi wa
promosheni ya tamasha la Fiesta litakalofanyika mkoani Mwanza ijumaa
hii.
Meneja
Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa
watatoa gari aina ya Vitz kwa mpenzi wa Fiesta atakayeshiriki katika
tamasha hilo kwa kutuma neon Fiesta kwenda namba 15678 na kuigingia
katika bahati nasibu hiyo.
Rodney
alisema kuwa mbali ya kushinda gari, mshiriki pia anaweza kushinda
fedha taslimu kiasi cha shs 100,000 kwa siku. Pia mpenzi wa Fiesta
anaweza kushinda pikipiki.
Mshindi
wa mkoa wa Mwanza atakuwa wa pili kupata gari ambapo mshindi wa kwanza
wa gari alikuwa Abdallah Ally Ngagari (51) aliyeshinda kupitia tamasha
la fiesta la Kigoma.
“Tumepania
kutoa zawadi katika mikoa yote ambayo Fiesta itafanyika, tumetenga
zaidi ya sh milioni 80 ili kufanikisha zoezi hili ambapo magari aina ya
vitz yapo nane kwa ajili ya kuwapa mashabiki, tunawaomba mashabiki
kushiriki kwa nguvu zote,” alisema Rodney.
Wakati huo huo; mkazi wa Shinyanga Rose Mahenda amafanikiwa kushinda pikipiki baada ya kushiriki katika bahati nasibu hiyo.
0 comments:
Post a Comment