Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
MAAFANDE
wa jeshi la Magereza, Tanzania Prisons “Wajelajela” wamewaomba
mashabiki wa jiji la Mbeya kujitokeza kwa wingi kuwapa hamasa katika
mchezo wao mkali na wakukata na shoka wa ligi kuu soka Tanzania bara
dhidi ya Mabingwa watetezi, klabu ya Yanga, keshokutwa uwanja wa sokoine
Mbeya.
Akizungumza kwa njia ya simu na mtandao wa FULLSHANGWE,
katibu mkuu wa Tanzania Prisons, Inspecta Sadick Jumbe amesema wanajua
wazi Mbeya ina watu wengi wanaopenda soka, na ndio maana walijitokeza
kwa wingi zaidi katika mchezo wa ndugu zao Mbeya City dhidi ya Yanga,
hivyo wajitokeze hata mwenye mchezo wao.
“Mbeya
City ilishangiliwa na umati mkubwa wa watu, mashabiki waje na kwenye
mchezo wetu dhidi ya Yanga ili tuwe pamoja kusaka ushindi wa kwanza
katika mchezo wa kwanza uwanja wa nyumbani”. Alisema Jumbe.
Jumbe
alisema wameanza ligi kwa mechi tatu za ugenini, hakika ilikuwa kazi
ngumu sana kwao na sasa wanarejea nyumbani kucheza mechi ngumu zaidi na
mabingwa watetezi, lakini wamejiandaa kushindana kwa nguvu zote ili
kupata matokeo ya ushindi.
“Yanga
ni timu bora na ndio mabingwa watetezi, wana wachezaji wazuri, lakini
mwaka jana tulitoka nao suluhu uwanja wa Sokoine na walitufunga Dar es
salaam, mwaka huu tunaanza nao tena nyumbani, hakika tutakomaa vibaya
sana na kufuta matokeo mabaya ya awali”. Alisema Jumbe.
Katibu
huyo alisema mashabiki wameanza kupoteza imani na kikosicha Jumanne
Chale na kuamini kuwa huenda kikafanya vibaya zaidi msimu huu, lakini
amewaondoa shaka kuwa ligi bado ni mbichi na timu inazidi kuimarika
kuanzia mchezo dhidi ya Coastal Union jumamosi.
“Mechi
ya Coastal tulikuwa na uwezo wa kushinda mabao matatu, lakini nao
waamuzi walichangia kutunyima ushindi, tulinyimwa penati za wazi na goli
moja tulilozamisha nyavuni, lakini yote kwa yote mwamuzi ndio mtu wa
mwisho, tulikubali na sasa tunasonga mbele.”. Alisema Jumbe.
Kwa sasa Tanzania Prisons wapo nafasi ya pili toka mkoani kwa kujikusanyia pointi moja tu katika mechi tatu za kwanza.
0 comments:
Post a Comment