Mahmoud Ahmad Arusha
Kocha
mkuu wa timu ya taifa(TAIFA STARS)Kim Poulsen amesema kuwa msingi mzuri
wa timu ya taifa unaanzia kwa vijana kupewa mafunzo ya soka angali
wakiwa bado wadogo na kupata makocha wenye utaalamu wa soka kuwafundisha
soka vijana hao iliwaje kuwa mabalozi wazuri wa timu ya taifa kwa siku
za usoni.
Poulsen
amesema hayo jijini hapa leo wakati alipokuwa balozi wa heshima kwenye
uzinduzi wa ligi ya Moivaro youth kwenye viwanja vya shule ya kimataifa
ya moshi iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha na kutanabaisha kuwa ligi
hiyo ni njia sahihi ya kupata wachezaji wa timu ya taifa kwa kuwa kituo
hicho kinachoendesha ligi hiyo kimekuwa kikifundisha kozi za awali na
kati kwa walimu wa soka na hiyo ni misingi imara ya soka.
Akawataka
wadau mbalimbali hapa nchini kuiga mfano huo katika juhudi za kukuza
soka la vijana kwa kutoa misaada ya vifaa na fedha za uendeshaji wa soka
hilo ilikukuza vipaji lukuki vilivyopo hapa nchi ilikujenga msingi
imara wakuwa na timu ya taifa hapo usoni itakayokuwa imeandaliwa
kiutaalamu tokea chini hadi timu ya taifa.
“unajua
hapa nimeona vijana wawili watakao kuwa msaada kwa timu ya vijana kama
watapewa mafunzo ya kiutaalam na ninaamini kuwa kwa makocha niliowaona
hapa hilo linawezekana ili klabu hii imenifurahyisha na kunitia moyo
kuwa msingi wa soka na vifaa wanavyopewa vijana vinaonyesha vipo
kitaalamu na vitasaidia ujenzi wa soka la kisasa kwa wachezaji hawa wa
siku za usoni”alisema Kim
Nae
Mkurugenzi wa Future Stars Alfed Itael amesema kuwa ligi hiyo
itaendeshwa kwa nyumbani na ugenini na timu zaidi ya 30 zinashiriki
mashindano hayo na kubainisha kuwa ligi hiyo itadumu kwa kipindi cha
kuanzia leo hadi mwezi wa March mwakani atakapopatikana Bingwa wa ligi
hiyo.
Itael
alisema kuwa ujio wa kocha mkuu wa taifa stars ni muendelezo wa kuwapa
changamoto vijana wanaoshiriki ligi hiyo kupata hamasa ya kujua majukumu
yao uwanjani kwani soka ni sehemu ya ajira kwa vijana hao kujituma
iliwaandae msingi wa soka lao siku za baadae akawataka vijana kuitumia
ligi hiyo kuweza kuweka msingi wa soka la kisasa kwa kufuata maagizo ya
walimu wao.
Ligi
hiyo pia ilizikutanisha timu za New Vision na FutureStars akatika mechi
ya ufunguzi na timu ya future stars kuibugiza new vision kwa mabao
matatu kwa nunge katika mtanange wa kukata na shoka uliopigwa baada ya
ufunguzi wa ligi hiyo iliyoonyesha ushundani kwa timu mbali mbali
zilizopata kushiriki siku ya leo.
Akizungumza
baada ya mechi hiyo mmoja wa vijana mwenye umri wa miaka 13 Yasin
Hashimu wa timu ya New Vision alisema kuwa mashindano hayo ni mazuri na
yatamsaidia kufikia malengo yake ya kuwa machezaji wa kimataifa kwa siku
za usoni na kuwa kufungwa kwa ni sehemu ya mchezo na wanaenda kujipanga
kuhakikisha mechi inayofuata wanatoa upinzani kwa timu watakayokutana
nayo.
Hashimu
akawataka wachezaji wenzake kufuta ushauri na mafunzo wanayopewa na
walimu wao ilikuwa wachezaji tegemeo kwa timu zao hapo baadae kwani soka
ni ajira na inajenga miili yetu na kutoa burudani kwa watazamaji kokote
ulimwenguni.
0 comments:
Post a Comment