Thursday, September 26, 2013


 
Promota wa Mpambano wa Ubingwa wa UBO Kaike Siraju katikati akiwanyoosha mikono juu mabondia Ramadhani Shauri kushoto na Cosmasi Cheka watakaopigana tarehe 27 Mwezi wa kumi  jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 
PAMBANO lingine la masumbwi linatarajia kufanyika Oktoba 27 katika ukumbi wa Friends Coner  Manzese Dar es salaam baina ya mabondia Ramadhani Shauri na Cosmas Cheka.
pambano hilo limedhaminiwa na Hotel ya Tanamera ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. 
Akizungumza mratibu wa pambano hilo,  Kaike Siraju amesema amepata sapoti kutoka hotel hiyo ili aweze kuendeleza vipaji vya vijana.
“Utakumbuka mimi ndiye ninayeandaaga mapambano makubwa nchini, lakini nilisimama kidogo kwa ajili ya kutafakari na kurekebisha mambo yangu binafsi ila kwa sasa nimekuja kuinua mchezo huu kwa vijana chipkizi”. Alisema Siraju.
Aliongeza kwa kutaja mapambano ya utangulizi kuwa ni Mohamed Matumla ambaye atamenyana na Sadiki Momba,  huku Amosi Mwamakula akizichapa na Hamisi Ajali na Juma Fundi atazipiga na Shabani Kilumbelumbe
 
Pia Siku hiyo kutakuwa  na uuzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Manny Paquaio, Saul ‘canelo’ alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kutakuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye amehaidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa hali ya juu wa kutupiana masumbwi

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video