Na Boniface Wambura, TFF
Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Azam na Yanga lililochezwa
jana (Septemba 22 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 138,188,000.
Watazamaji
waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 33 la VPL msimu wa
2013/2014 lililomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 3-2
walikuwa 24,020.
Viingilio
katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 33,065,409.1 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 21,079,525.42.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 16,812,919.89,
tiketi sh. 5,022,342, gharama za mechi sh. 10,087,751.93, Kamati ya Ligi
sh. 10,087,751.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
5,043,875.97 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 3,923,014.64.
Mechi iliyopita ya VPL kwenye uwanja huo kati ya Simba na Mbeya City iliingiza sh. 123,971,000.
MECHI YA TOTO, POLISI DOM KUPIGWA J2
Mechi
namba 12 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Toto Africans na Polisi
Dodoma iliyokuwa ichezwe Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza imesogezwa mbele kwa siku moja.
Timu
hizo za kundi C sasa zitapambana Jumapili (Septemba 29 mwaka huu)
kwenye uwanja huo huo ili kupisha mechi namba 10 kati ya Pamba na Stand
United FC ya Shinyanga itakayochezwa Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu).
Mechi
nyingine za kundi hilo zitakazochezwa Jumamosi ni Mwadui na Polisi
Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) wakati Kanembwa JKT na Polisi
Mara zitacheza kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
0 comments:
Post a Comment