JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
|
|
|
Simu: +255-22-2112035/40
|
S.L.P. 9223
|
|
Nukushi: +255-2122617/2120486
Barua Pepe: [email protected]
|
Dar es Salaam
Septemba 19,2013
|
Operesheni Kimbunga na usakaji wahalifu katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Julai 29, 2013 aliagiza kufanyika operesheni maalum iliyopewa jina la
Operesheni Kimbunga yenye lengo la kuondoa uhalifu katika mikoa ya
Kagera, Kigoma na Geita ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na kuwepo
kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.
Operesheni
hii pamoja na kufanikiwa kuondosha nchini kwa lazima jumla ya wahamiaji
haramu 7,819 kuanzia Septemba 6, 2013 hadi kufikia Septemba 17, 2013,
imeweza kushughulikia uhalifu na kufanikiwa kukamata majambazi wa
kutumia silaha, majangili, mabomu ya kutupwa kwa mkono , bunduki za aina
mbali mbali, Risasi, mitambo ya kutengeneza bunduki aina ya magobole,
Sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, na kibuyu cha maji cha Jeshi
hilo.
Jumla
ya watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha 55 pamoja na mabomu ya
kutupwa kwa mkono (8), silaha 47 zikiwemo bunduki aina ya SMG( 4), Shot
gun (4), Bunduki aina ya Riffle (2), Bunduki aina ya Mark IV (1),
Bunduki aina ya Gobole (37) zimekamatwa wakati wa operesheni Kimbunga
hadi kufikia Septemba 17,2013 katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Aidha,
risasi (602) zilikamatwa zikiwemo Risasi (500) za bunduki ya aina ya
SMG na SAR, Risasi (20) za bunduki aina ya Mark IV na risasi (82) za
bunduki aina ya Gobole, fataki (8), mitambo ya kutengeneza magobole (2),
misumeno ya kukata miti ( 9), Mbao (1,516), Magogo (86), na mkaa
magunia (111).
Aidha,
Watendaji wa Operesheni Kimbunga pia wamefanikiwa kukamata jumla ya
majangili Watanzania (3), Vipande vya meno ya Tembo (2), Ngozi za
wanyama mbali mbali wakiwemo Nyati (1), Duma (1) na Swala (2). Pia
walikamata nyama ya porini, magunia ya bangi (6), Gongo lita (86) na
lami mapipa (10).
Wakati
huo huo, Ng’ombe 3,436 wamekamatwa baada ya wafugaji haramu
kutelekeza mifugo hiyo wakati walipozingirwa na timu ya operesheni
kimbunga katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Kumekuwepo
na tabia ya baadhi ya wamiliki wa mifugo kutoka nchi jirani ambao wengi
wao ni matajiri na viongozi serikalini kuwatuma watumishi wao kuingiza
mifugo katika ardhi ya Tanzania hususan kwenye hifadhi ya Taifa kwa
ajili ya malisho na watumishi hao hupewa silaha kwa ajili ya kujihami
wakiwa kazini.
Mifugo imekuwa ikiharibu mazingira na kuleta migogoro ya ardhi katika mikoa hii.
Operesheni Kimbunga itahakikisha inawakamata wahalifu wote wanaotishia amani hususan katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Aidha,
wananchi ambao ni raia pamoja na Raia wenye asili ya nchi jirani
wanaowakaribisha na kuwahifadhi wahalifu na wahamiaji haramu watakamatwa
na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mhamiaji
haramu ni raia yeyote wa kigeni aliyeingia na kuishi nchini bila
kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria ya Uhamiaji namba 7 ya mwaka
1995.
Utaratibu
chini ya Sheria hiyo unamtaka raia wa kigeni anayeingia nchini kuwa na
Hati ya kusafiri, kuripoti katika vituo halali vya kuingilia nchini na
kujaza fomu za uhamiaji za kuingia nchini.
Aidha,
Raia wa kigeni anayehitaji kuishi nchini analazimika kuwa na hati za
ukaazi itakayomruhusu kufanya shughuli iliyomleta mfano biashara,
matembezi, uwekezaji, Kusoma, matibau, kufanyakazi nakadhalika.
Operesheni
Kimbunga inayoongozwa na Brigedia Jenerali Mathew Sukambi imeanza rasmi
Septemba 6, 2013 baada ya kutoa muda wa wiki Mbili kwa wahamiaji
wanaoishi nchini bila kufuata sheria kuondoka kwa hiari.
Taarifa
hii imetolewa na Zamaradi Kawawa, Kiongozi wa Timu ya Habari na
Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga. Septemba 19, 2013, Biharamulo,
Kagera. Kwa maelezo zaidi piga Simu namba 0754698856, Email;
[email protected]
0 comments:
Post a Comment