JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Operesheni Kimbunga haikuondoa Wakimbizi nchini kama ilivyoripotiwa na baaadhi ya Vombo vya Habari vya hapa nchini na vya nje.
Ifahamike
kuwa zoezi hili limehusisha Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani
(UNHCR) ili kuhakikisha kuwa wakimbizi hawahusishwi katika zoezi la
kuondoshwa nchini.
Kwa
mujibu wa tafsiri iliyotolewa na Mkataba wa Kimataifa wa mwaka 1951
kuhusu hadhi ya Wakimbizi, Mkimbizi ni mtu anayekimbia nchi yake kwa
hofu ya maisha yake kuwa hatarini kwa sababu za kikabila, dini, utaifa,
uanachama wa chama cha kijamii au kisiasa na kufuata hifadhi katika
nchi nyingine.
Mkimbizi
anapokimbilia katika nchini nyingine kuomba hifadhi ana haki ya kupewa
hifadhi na kuhakikishiwa usalama wake. Pia ana haki ya kupokelewa na
kutorudishwa katika nchi ambayo ameikimbia.
Hivyo , kutokana na Mkataba huo, Tanzania wakati inatekeleza Operesheni Kimbunga haikumgusa mkimbizi.
Aidha,
ieleweke kuwa yapo mazingira ambapo hadhi ya mkimbizi hukoma pale
ambapo suluhisho la kudumu la matatizo ambayo yalimfanya mkimbizi
kukimbia nchi yake limepatikana na hivyo mkimbizi mwenyewe kutaka kurudi
nchini kwake kwa hiari ama pale mkimbizi anapohamishiwa kwenye nchi ya
Tatu kwa makubaliano maalum na pale ambapo mkimbizi anapewa uraia au
ukaazi wa nchi iliyompatia hifadhi.
Hivyo
basi, mkimbizi anaweza kuwa mhamiaji haramu pale ambapo hakurudi katika
nchi yake kwa hiari baada ya kupatikana suluhisho kwa matatizo
yaliyosababisha kukimbia ama hakupata fursa ya kwenda nchi ya Tatu na
hakuomba Uraia au ukaazi wan chi iliyokuwa inampa hifadhi.
Ieleweke
kuwa Mkimbizi ambaye alirudi nchini kwake kwa hiari yake na baadaye
kuamua kurudi katika nchi iliyokuwa inamhifadhi hawezi kuendelea kuwa na
hadhi ile ile ya ukimbizi . Mtu huyu anatakiwa kufuata Sheria ya
Uhamiaji namba 7 ya 1995. Iwapo ataishi nchini bila kufuata sheria hiyo
atahesabika kuwa mhamiaji haramu.
Inawezekana
kuna watu ambao hadhi yao ya ukimbizi imekoma na wanaishi nchini isivyo
halali wakakumbwa na Operesheni Kimbunga na kudai kuwa wao ni
wakimbizi.
Juhudi za Serikali za kuwataka wahamiaji haramu kuhalalisha ukaazi nchini kwa hiari
Kwa
vipindi tofauti, Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji iliendesha zoezi la
kuhamasisha watu wanaoishi nchini isivyo halali kurudi nchini kwao
kutokana na hali ya usalama katika nchi hizo kuimarika. Aidha, kwa
waliotaka kubaki na kuendelea kuishi nchini walielekezwa kufuata sheria
na taratibu za Uhamiaji.
Utafiti
uliofanywa na Mradi wa Kimataifa wa kushughulikia masuala ya kiuhamiaji
ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unaoongozwa na Prof. Boneventure
Rutinwa 2006/2007 katika mkoa wa Kagera unaonyesha kuwa Wilaya ya
Karagwe pekee Inakadiriwa kuwa na wahamiaji haramu 30,850 lakini pamoja
na kuhamasishwa kuhalalisha ukaazi wao, watu 2,000 pekee walifuata
taratibu walizoelekezwa na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji ili kuhalalisha
ukaaji wao nchini.
Pamoja
na juhudi zote za Serikali za kuhamasiha wahamiaji haramu kuhalalisha
ukaazi wao nchini bado hawakufuata taratibu na badala yake utafiti
unaonyesha kuwa waliendelea kuingia na kuhamia katika wilaya nyingine
mfano Biharamulo na maeneo mengine.
Taarifa
hii imetolewa na Zamaradi Kawawa, Kiongozi wa Timu ya Habari na
Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Septemba 20,2013, Biharamulo,
Kagera. Kwa maelezo zaidi Email: [email protected].
0 comments:
Post a Comment