JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Operesheni
Kimbunga inayoendelea katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita hailengi
kuondoa wahamiaji haramu kutoka taifa moja na hadi Septemba 20, 2013,
imefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 9,283 toka nchi za Rwanda, Burundi,
Uganda, Somalia, DRC Congo, Yemen na India.
Idadi
kubwa ya wahamiaji hawa haramu waliokamatwa ni kutoka Burundi (5,355)
wakiafuatiwa na Rwanda (2,379), Uganda (939), DRC Congo (564), Somalia
(44), Yemen (1) na India (1).
Takwimu
zinaonyesha kuwa mkoa wa Kigoma unaongoza kwa idadi kubwa ya wahamiaji
haramu waliondoshwa nchini ikiwa na jumla ya wahamiaji haramu (4,365)
ukifuatiwa na mkoa wa Kagera wenye ambapo walikamatwa wahamiaji haramu
(4,335) na Geita (583).
Operesheni
Kimbunga ilianzishwa kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya uhalifu
vilivyokithiri vikiwemo ujambazi wa kutumia silaha,ujangili, utekaji wa
magari na mauaji ya kikatili pamoja na migogoro ya ardhi inayotokana na
wafuagaji kutoka nchi jirani kuingiza mifugo yao kwa ajili ya malisho.
Aidha,
jumla ya wahamiaji haramu 3,238 waliondoshwa nchini kwa amri ya
Mahakama baada ya kupewa hati ya kufukuzwa nchini wakati wananchi
wengine 1,108 waliokuwa wanachunguzwa kama kweli ni raia wa Tanzania
waliachiwa huru baada ya watendaji kuthibitisha kuwa ni raia halali
wakati huo huo wengine 1,303 wakiwa wanaendelea na uchunguzi ili
kuthibitisha uraia wao.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Julai 29, 2013 aliagiza kufanyika kwa opereheni maalum ya kuondoa
uhalifu katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita mbao kwa kiasi kikubwa
umechangiwa na kuwepo kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.
Operesheni
Kimbunga inayoongozwa na Brigedia Jenerali Mathew Sukambi imeanza rasmi
Septemba 6, 2013 baada ya kutoa muda wa wiki mbili kwa wahamiaji
wanaoishi nchini bila kufuata sheria kuondoka kwa hiari yao au
kuhalalisha ukaazi wao nchini.
Taarifa
hii imetolewa na Zamaradi Kawawa, Kiongozi wa Timu ya Habari na
Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Septemba 20,2013, Biharamulo,
Kagera. Kwa maelezo zaidi Email: [email protected].
0 comments:
Post a Comment