Paroko
wa Parokia ya Roho Mtakatifu Cheju Zanzibar, akisaidiwa na Frateri,
Richard Haki kupumzika kitandani baada ya kuzungumza na waandishi katika
katika Wodi ya Kibasila iliyopo katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) jijni Dar es Salaam jana.Picha Salim Shao
…………….
Dar es Salaam/Zanzibar.
Padri wa Parokia ya Mpendae ya Kanisa Katoliki Zanzibar, Anselmo Mwang’amba amesema kuwa alimwona mtu aliyemwagia tindikali na kumsababishia majeraha na kueleza kuwa anashangaa kuona polisi hawajamkamata hadi sasa.
Padri wa Parokia ya Mpendae ya Kanisa Katoliki Zanzibar, Anselmo Mwang’amba amesema kuwa alimwona mtu aliyemwagia tindikali na kumsababishia majeraha na kueleza kuwa anashangaa kuona polisi hawajamkamata hadi sasa.
Akizungumza jana katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwenye Wodi namba 16, Kibasila
alipolazwa, Padri Mwang’amba alisema baada ya kumwagiwa tindikali,
alimwona mtu huyo akikimbia kuelekea katika nyumba moja jirani.
“Kwa kuwa mimi nilikuwa na
taharuki na maumivu, sikuweza kuendelea kumfuatilia, ila dereva
aliyenikimbilia kunipa msaada aliniambia kwamba alimwona mhusika
akikatiza kwenye uchochoro hadi alipoingia kujificha kwenye nyumba
iliyopo jirani na eneo hilo,” alisema.
Alisema majeraha aliyoyapata
wakati akitokea katika duka la huduma za mawasiliano ya mtandao la Shine
Shine saa 10.15 jioni, ambayo yanamsababishia maumivu makali, hayawezi
kumfanya aikimbie Zanzibar, kwa kuwa hata Yesu Kristo wakati alipokuwa
katika kazi za utumishi duniani alipata mateso makali kuliko yake.
“Nilisomea upadri nikiwa
Zanzibar kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1981 nilipopata upadrisho kamili.
Niko huko kwa kazi ya Mungu wala si mwanadamu, kwa hiyo nikitoka hapa
narejea hukohuko, siogopi, ingawa miaka hiyo nilipokuwa naanza kazi hii
hakukuwa na mambo kama haya,” alisema.
Aliwataka Wakristo wanaoishi
Zanzibar kuendelea kuwa na umoja na upendo pamoja na kuwa makini kwa
usalama wao licha ya matukio magumu yanayowakuta ikiwamo vitisho na
kuchomwa moto kwa makanisa.
Pia aliunga mkono shinikizo la
kutimuliwa kazi kwa Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa
kutokana na kushindwa kuwakamata watu wanaomwagia watu tindikali.
“Huyu bwana alishindwa hata
kunijulia hali wakati nikiwa hospitali huko Zanzibar, tofauti na
nilipokuja Bara ambako Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
walifika kunijulia hali na kuzungumza nami hospitali.
“Kwa hali hii, naona kwamba
tukio langu ni la kupangwa na litazungumzwa sana lakini baada ya muda
halitashughulikiwa. Atajeruhiwa mwingine tena lakini hatua za dhati za
kudhibiti ukatili huu usiendelee hazijachukuliwa. Mimi ni padri wa tatu
kufanyiwa ukatili,” alisema.
Mapadri wengine ni Ambros Mkenda aliyepigwa risasi na kujeruhiwa wakati Padri Evarist Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi.
Al-Shabaab wanaswa Zenji
Katika
hatua nyingine, Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watu wanaodaiwa
kuwa wafuasi wa kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab cha Somalia.
CHANZO: GAZETI LA MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment