Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa wilaya ya Bariadi kwenye Viwanja vya Sabasaba.
~. Adai wamechukizwa na viwanda vya nguo,nyuzi ,nyama na ajira.
~. Asema misaada ya China ni ukombozi mkubwa unaowakera Chadema.~. Awataka kanda ya ziwa kuujua unafiki huo wa Chadema.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye ameeleza kusikitishwa kwake
na hatua ya Chadema kukerwa na hatua za Balozi wa China na serikali ya
China kwa ujumla katika kushiriki katika hatua za kuwakwamua watanzania
katika umasikini.
Nape
alisema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji wa Bariadi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM sabasaba
Mkoani Simiyu.
Alisema
hoja kuwa ambayo imewakera na kuwasumbua Chadema ni hatua
zinazochukuliwa hivi sasa kwa pamoja kati ya Serikali ya CCM na Serikali
ya China ambayo hivi sasa inaelekea kuzaa matunda ya kutoa mwanya wa
ajira zaidi ya elfu- 25 viwandani.
“Tayari
tushaingia makubaliano na serikali ya China ya kuwekeza katika viwanda
vya kuongeza thamani ya mazao kama Pamba, ufuta, alzeti na mazao ya
mifugo ikiwemo ngozi za ng’ombe, hivyo wananchi, chuki na hasira ya
Chadema dhidi ya Balozi wq China inasababishwa na mafanikio hayo ya
kutatua matatizo ya wananchi” alisema Nape.
“ushahidi
wa hasira za Chadema unadhihilishwa na ukweli kwamba tayari wawekezaji
wa viwanda hivyo vya kuongeza thamani ya mazao washawasili nchini na
wengine wameshaanza ujenzi wa viwanda hivyo mjini Shinyanga, na kwamba
vitaanza kazi ya uzalishaji mwezi desemba mwaka huu” Aliongeza.
Nape
aliwataka watanzania kuzipuuza shutuma za Chadema dhidi ya Balozi wa
China na kusisitiza kuwa hasira yao imesababishwa na hofu ya mtaji wao
wa kutumia udhaifu na umasikini wa watanzania hasa vijana wasi na ajira
kama mtaji wao wa kisiasa.
“Chadema
wamehanganyikiwa, kwa sababu siku zote wamekuwa wakitegemea kuendesha
chama chao kwa mgongo wa umaskini wa watanzania, sasa kasi ya
kutengeneza ajira kupitia ujenzi wa viwanda, na mchakato wa kuwezesha
kuongeza bei ya mazao ili kuwakwamua wakulima kutoka katika umaskini
umewachanganya” Alisisitiza Nape.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita Balozi wa China alishiriki katika ziara ya Katibu
Mkuu wa CCM Abdurlahaman Kinana kwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa
viwanda vinavyojengwa na wawekezaji toka nchini China katika mikoa ya
kanda ya ziwa ikiwemo vile vinavyojengwa mjini Shinyanga jambo
linalolalamikiwa na Chadema
0 comments:
Post a Comment