Sunday, September 1, 2013

1Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philip Mulugo akimuangalia mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Premier Rehema Ng’anzi,  anayeonesha kwa vitendo mambo ya kisayansi wanayosoma shuleni kwao, wakati alipotembelea banda la shule hiyo kwenye maonesho ya Vodacom Elimu Expro.
2Naibu Waziri Mulugo akimsikiliza Mkurugenzi wa JUE INTER SCHOOLS Ester Alexander kutoka Arusha wakati  akimueleza juu mambo yanayofanywa na shule yake.
3Elizabeth Thomas (aliyeshika kipaza sauti) kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala akimueleza Naibu  Waziri Mulugo kuhusu Tamasha la Mnazi Mkinda  linaloandaliwa na halmashauri hiyo kuboresha sekta ya elimu katika eneo hilo.
4Mwanafunzi Wycklif Michael anayesoma kidato cha sita Shule ya Sekondari ya Loyola, akimuonesha Naibu Waziri Mulugo programu ya mfumo wa kupiga kura aliyoibuni.
8Naibu Waziri Mulugo akizungumza na hadhira(haipo pichani) kwenye maonesho hayo
Hussein Makame, MAELEZO
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philip Mulugo ameitaka jamii kupiga vita matumizi mabaya ya simu za mikononi, kompyuta na mitandao ya kijamii yenye muelekeo hasi kwa mustakbali wa taifa la Tanzania.
Waziri Mulugo ameyasema hayo wakati akizindua maonesho Vodacom Elimu Expro 2013 yaliyofanyika  kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Lengo la maonesho hayo ni kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali za kielimu miongoni mwa wanafunzi, walimu, wakufunzi,wahadhiri na jamii nzima ujumla kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Alitoa wito kwa wazazi, walezi na jamii yote kutumia teknolojia ya elimu masafa na mitandao kwa matumizi mazuri ya kupata taarifa za kitaaaluma na kimaendeleo bila kuangalia mitandao ambayo watu wengine hutukana matusi ya nguoni, kuangalia picha ngono na mambo mengine yenye muelekeo hasi.
“Tunasema ni jukumu letu sisi sote kulinda mila na desturi zetu kama Watanzania pamoja na maadili ya watoto wetu na vizazi vyetu kama nchi yetu ya Watanzania ilivyo, taarifa zinazowekwa kwenye mtandao ziwe sahihi ili zisiwapotoshe watoto na vijana kwenye shule na vyuo vikuu.” alisema Waziri Mulugo.
Akifafanua kuhusu suala la wanafunzi kuwa na simu, Waziri Mulugo alisema si kosa kwa mwanafunzi kuwa na simu maadam anaitumia kwenye matumizi chanya.
“Lakini asiingie na simu darasani na mimi nitakuwa mtu wa kwanza nikimkuta mwanafunzi ana simu namnyang’anya ili tuweze kuwajenga watoto kwenye maadili kwa sababu wanatumia simu kwenye matumizi hasi, ujumbe wa kimapenzi, mitandao ya picha za ngono n.k”alisema Waziri Mulugo na kuongeza:
“Sisi kama Serikali tunalinaoinda maadili ya watoto hatuwezi kuruhusu jambo hili kwa hiyo naomba mwanafunzi anapotumia simu atumie kwa matumizi  chanya, aangalie ‘material’ kama ambavyo nia ya maonesho ya leo yalivyo, tusipotoshe umma”  
Akizungumzia lengo la maonesho hayo na malengo ya Serikali, Waziri Mulugo alisema kuwa Tanzania inahitaji elimu bora tena kwa nguvu sana kwani kuna shule nyingi, vyuo vikuu na vya kati vimeanzishwa, hivyo ni lazima wanafunzi wapate taarifa  kamili tena zilizo sahihi na zinazoeleweka.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video