STRAIKA
wa Simba, Betram Mwombeki ametamka kwamba kiungo Henry Joseph Shindika
ni bonge la mchezaji na tangu aanze kuichezea Simba iwe kwenye ligi au
mazoezi amegundua vitu vingi kwake.
“Kuna viungo wengi Simba,
nawakubali uwezo wao kila mmoja na mchango kwenye timu, lakini
kilichonivutia zaidi ni uwezo wa Henry anapokuwa uwanjani, ana nguvu,
akili, uzoefu na ameuzoea mpira. Anajua ni wapi akuwekee mpira kutokana
na kasi na mbinu ulizonazo mshambuliaji,” alisema Mwombeki.
“Naamini tukizidi kuwa naye
karibu tutajifunza mengi na pia tutapata mabao mengi pamoja na ubingwa
wa ligi msimu huu kirahisi zaidi, anajua wapi pa kumuwekea straika mpira
afunge,” alisema Mwombeki mwenye malengo ya kufunga jumla ya mabao 27
msimu huu wa ligi.
Mwombeki alifunga bao la pili kwenye mechi ya ligi Jumamosi iliyopita dhidi ya Mtibwa huku la kwanza likifungwa na Henry Joseph.
CHANZO: MWANASPOTI
0 comments:
Post a Comment