Baadhi
ya raia wa Nigeria wanaodaiwa kutunzwa Mwinjilisti mwanamke mwenye
kibali cha kazi hiyo Blessing Dangana katika huduma ya Life Changer
Chapel iliyoko Sinza jijini Dares Salaam , wakitoka nje ya Mahakama
ya Hakimu Mkazi ya Kisutu mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo huku
wengine wa kijificha sura zao.
Baadhi
ya vijana wanaodai kuwa wanatoka mkoa wa Kigoma wakiwa wajaza fomu
leo ambao taarifa zao zinaendelea kuchunguzwa kama kweli ni
Watanzania wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dares Salaam.
Gari
la Idara ya Uhamiaji likiwa limebeba baadhi ya raia wa Nigeria
wanaodaiwa kutunzwa Mwinjilisti mwanamke mwenye mwenye kibali cha
kazi hiyo Blessing Dangana katika huduma ya Life Changer Chapel
iliyoko Sinza jijini Dares Salaam hao mara baada ya kutoka mahakama ya
Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dares Salaam.
Mwiinjilisti
mwanamke kutoka nchini Nigeria ambaye ana kibali cha kazi ya
uinjilisti katika huduma ya Life Changer Chapel iliyoko Sinza
jijini Dares Salaam , Blessing Dangana, anayedaiwa kuwatunza raia wa
Nigeria watano ambao wanatoa huduma hiyo bila kibali maalum akitoka nje
ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu mara baada ya kufikishwa
mahakamani hapo leo.
Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo
0 comments:
Post a Comment