Saturday, September 7, 2013


001Huyu ndiyo Mtuhumiwa Musa Senkando anayetafutwa na polisi. 
002Marehemu Yusta Mkali enzi za uhai wake
003Polisi wa kituo cha kawe akiukagua mwili wa marehemu Yusta Mkali
004Wakazi wa Kawe wakiwa na nyuso za huzuni wakati mwili wa marehemu ukitolewa ndani kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
005Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukitolewa kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala
Na Mwandishi wetu.
Mkazi wa Kawe Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Musa Senkando anatafutwa na polisi kwa mahojiano baada ya kutoweka akisadikika kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina la Yusta Mkali.
Mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo (jana) , huku habari za kuaminika za mauaji hayo kutendeka zikithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura ambaye  alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema  uchunguzi wa awali wa mauaji hayo unaonesha kuwa  yanasadikika kutokea usiku wa kuamkia(leo) jana.
“Yusta ameuwawa na kitu chenye ncha kali kilichomchoma kwenye koromeo na inasadikika mume huyo ameshatoweka na jeshi la polisi linamtafuta kwa uchunguzi zaidi kwani yeye ndiye aliekuwa mtu wa mwisho kuwa nae ndani,” alisema.
Wambura alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi. 
Naye Mtoto wa dada yake marehemu ambaye alikuwa anaishi naye, Joshua Zebedayo alisema yeye ameshtukizwa na mauaji hayo pale alipo amka asubuhi kuelekea kufanya usafi chumbani mwa mama yake mdogo kwani yeye huwa analala chumba kingine na ndipo alipoukuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha pamoja na damu.
“Ilikuwa majira ya saa mbili asubuhi nilipoamka kufanya usafi chumbani kwa mama kama ilivyokawaida yangu mama na baba waendapo kazini, ila cha kushangaza nilimkuta mama bado amelala wakati alitakiwa kuwepo kazini. Nilimwita mama bila mafanikio nikafunua shuka alilojifunika na kumkuta amekwisha fariki dunia,” alisema kijana huyo huku akibubujikwa na machozi.
Marehemu Yusta wakati wa uhai wake,alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya umma Frontline Porter Novelli(PR COMPANY)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video