.Serikali yadai kuchapisha habari, makala za uchochezi
Serikali imeyafungia Magazeti ya
Mwananchi na Mtanzania kuanzia juzi kutochapishwa kutokana na magazeti
hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya
kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha
amani na mshikamano ulipo nchini.
Tamko
la Serikali lililotolewa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, ilisema kuwa Gazeti la Mwananchi limefungiwa
kutochapishwa kwa siku 14 na Mtanzania siku 90.
Adhabu hiyo imetangazwa kwa tangazo la Serikali Namba 333 la juzi.
Tamko
hilo limesema gazeti hilo limepewa adhabu hiyo kutokana na kuchapisha
habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani, ambapo Julai
17, mwaka huu katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo
“MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa
matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa siri haukupaswa
kuchapishwa magazetini.
Aidha,
katika toleo la Jumamosi, Agosti 17, 2013 lilichapisha habari yenye
kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” “habari hiyo
ilikolezwa na picha ya mbwa mkali mwenye hasira. Habari na picha hiyo
ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka mbwa katika maeneo ya
ibada ya waumini wa dini ya kiislam. Jambo ambalo halikuwa la ukweli.”
Lilisema tamko hilo.
Lilisema
Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo
ya misikiti. Serikali na Jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia
maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au
kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
“Hivyo
basi, kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa
ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya
kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.”
Aidha,
tamko hilo lilifafanua kuwa gazeti la Mtanzania limefungiwa
kutochapishwa kwa siku 90 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi. “Gazeti
hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa
kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari.
Pamoja
na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa
Magazeti, mfano ; katika toleo na 7262 la 20 Machi, 2013 liliandika
habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”, tarehe 12 Juni, 2013,
toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Tamko
hilo liliongeza kuwa siku ya Jumatano, Septemba 18, 2013 katika toleo
Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha kichwa cha habari kisemacho
“SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo
unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi
nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika.”
Aidha,
katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la
Polisi linahusika na wahanga waliumizwa na watu wasiojulikana kwa
kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
“Kwa
ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi
wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii.
“Tamko
limesema Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kwa ujumla
kuwa makini, kuzingatia weledi, miiko na madili ya taaluma uandishi wa
habari.
“Serikali
inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakikisha kuwa habari
wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma, kuweka
mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.
“Serikali
inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu
kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwamo ya kuvifungia . Serikali
haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani
nchini.”
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
0 comments:
Post a Comment