TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 16. 09. 2013.
WILAYA YA MBARALI – MWALIMU AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUBAKA
WANAFUNZI WAWILI.
WANAFUNZI WAWILI.
|
§ MNAMO
TAREHE 13.09.2013 MAJIRA YA SAA 21:30HRS HUKO KATIKA SHULE YA SEKONDARI
MONTFORT WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ANDREW S/O SHADRACK, MIAKA
26,MKURYA, ALIYEKUWA MWALIMU WA SHULE YA SEKONDARI MONTFORT AKIFUNDISHA
MASOMO YA LUGHA YA KIINGEREZA NA MASOMO YA DINI AMBAYE HIVI SASA NI
MWALIMU KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWEMBENI – MUSOMA MKOANI MARA
ALIMBAKA, MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE SHULENI HAPO JINA LIMEHIFADHIWA,
MIAKA 17, MHEHE . MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMTOA DARASANI WAKATI AKIJISOMEA
“PREPO” NA KUMPELEKA GIZANI KISHA KUMBAKA KWA NGUVU HUKU AKIMPA AHADI
MBALIMBALI.
§ AIDHA
MAJIRA YA SAA 22:00HRS KATIKA SHULE HIYO MWALIMU HUYO ALIMBAKA
MWANAFUNZI MWINGINE WA KIDATO CHA NNE JINA LIMEHIFADHIWA, MIAKA 18,
MPARE. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMUITA KUTOKA BWENI AKIWA AMEPUMZIKA NA
KUMBAKA KWA NGUVU HUKU AKIMPA AHADI MBALIMBALI.
§ MTUHUMIWA
ALIKUWA AKIWARUBUNI WAHANGA KWA AHADI MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA
KUWAPA MSAADA KATIKA MASOMO KWA KUWA ATARUDI KATIKA SHULE HIYO MUDA SI
MREFU KUSHIKA WADHIFA WA MWALIMU MKUU.
§ MTUHUMIWA AMEKAMATWA, TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI LEO.
§ KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA TAMAA ZA KIMWILI NA MADHARA YA
KUFANYA MAPENZI [NGONO] ZEMBE KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO. AIDHA
ANATOA RAI KWA WATU WAZIMA KUACHA TABIA YA KURUBUNI /SHAWISHI WATOTO
WADOGO HUSUSAN WANAFUNZI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA, BADALA YAKE WAWE
WAAMINIFU KWA KUCHAGUA MWENZI MMOJA WA KUISHI NAE.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment