Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
MABINGWA
wa zamani wa ligi kuu nchini Tanzania, Wana TamTam, Mtibwa Sugar tayari
wameshaanza mawindo yao huko Mashamba ya miwa ya Manungu Turiani Mkoani
Morogoro dhidi ya klabu mpya ya Mbeya City keshokutwa uwanja wa Manungu
Complex.
Akiongea kwa njia ya simu jioni hii na mtandao wa MATUKIO DUNIANI,
Meneja wa klabu hiyo, David Bugoya amesema baada ya mchezo wa jumamosi
ya wiki iliyopita ambao walipoteza kwa kutunguliwa mabao 2-0 na Mnyama
Simba, kikosi kamili kimerejea jana Manungu na kuanza mazoezi.
Bugoya
amesema ligi bado ni mbichi, hivyo wanazidi kujipanga na kuhakikisha
wanafuta makosa yaliyojitokeza katika mechi za nyuma na kuangalia zaidi
mbele.
“Siku
zote kocha wetu, Mecky Mexime amekuwa akitamka kuwa soka ni mchezo wa
makosa, wachezaji wake walifanya makosa mbele ya Simba na kuadhibiwa,
lakini kwa sasa timu inaendelea na mazoezi hapa Manungu, na
ninavyokuambia muda huu kaka, nipo mazoezini kuwawinda Mbeya City”.
Alisema Bugoya.
Hata
hivyo Bugoya amesema kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika mchezo
wa Mbeya City dhidi ya Yanga uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, wameeleza
kuwa klabu hiyo inacheza soka safi na kuonesha kuwa wako hai kwa hali ya
juu.
“Nasikia
vijana hawa ni wazuri sana na waliwabana sana Yanga, lakini soka ni
mchezo wa mahesabu, chochote kinaweza kutokea. Sisi tunaendelea vizuri
na mazoezi yetu na wachezaji wana morali kubwa sana kwani wanajua ligi
bado ni mbichi sana”. Alisisitiza Bugoya.
Mpaka
sasa Mtibwa wamejikusanyia pointi 4 kibindoni na wapo nafasi ya 8
katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara, wakati Mbeya City wapo
nafasi ya 7 wakijikusania pointi 5.
Wakati
watengeneza sukari hao wa Manungu wakiendelea na jalamba, nao wakali wa
,Mbeya na kipenzi cha mashabiki mkoani humo, klabu ya Mbeya City
inatarajia kuwasili leo mkoani Morogoro tayari kwa mchezo huo ambao ni
wa kwanza kwao kucheza nje ya uwanja wao wa Sokoine.
0 comments:
Post a Comment