Tuesday, September 3, 2013

IMG 1Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki Adam Kimbisa akieleza kwa waandishi wa Habari sababu iliyopelekea wao kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati wa vikao vya bunge hilo, wakati wa mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Nderakindo Kessy.
IMG 2Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Nderakindo Kessy akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari wakati wa mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
IMG 3Katibu wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki Shyrose Bhanji akifafanua jambo kuhusu Msimamo wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo kuhusu vikao vya Bunge kufanyika kwa mzunguko, wakati wa mkutano na uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene
IMG 4
Baadhi wa waandishi wa habari wakiwasikiliza wabunge wawakilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
DONDOO MUHIMU ZA KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI 03/09/2013 – MAELEZO
Bunge la tatu la Afrika Mashariki lilikuta vikao vya Bunge vikifanyika kwa njia ya mzunguko kwa nchi 4 za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi) pamoja na Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya.
Katika kikao cha Kamati ya Uongozi, Wabunge wa Tanzania walitoa pendekezo kwamba vikao vya Bunge kwa mwaka huu wa fedha August 2013 –June 2014 vifanyike Arusha, kwa vile tayari kuna makazi ya kudumu yaani jengo jipya lililojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na kiwanja kilitolewa na Serikali ya Tanzania.

Hata hivyo Wabunge wenzetu walipendelea vikao vya Bunge viendelee kwa mzunguko na Wabunge Watanzania tuliendelea na msimamo wa vikao kufanyika Arusha.
Motion ililetwa Bungeni na mwenzetu kutoka Kenya kuhusu vikao vya Bunge kufanyika kwa mzunguko….Spika alimwambia mleta Motion kufuata kanuni ambapo ilitakiwa mjadala wake uendelee katika kipindi cha masaa 24 baada ya kuwasilisha.
Wabunge wenzetu hawakukubaliana na uamuzi wa Spika na kuamua kutoka nje na kusababisha kikao cha Bunge kuahirishwa mpaka siku inayofuata.
Kwa utaratibu wa kanuni za Bunge, iwapo nchi moja isipokuwa na Wabunge wasiozidi zaidi ya watu basi kikao cha Bunge kinavunjwa kwa dakika 15 na Bunge kuanza tena na baada ya hapo ikiwa bado akidi ikiwa haitosh, kikao cha Bunge huvunjwa mpaka siku inayofuata.
Wabunge wa Tanzania tuliamua kwa pamoja kuwa na msimamo wa kutoka ndani ya Bunge kwa kuonyesha kusikitishwa na kitendo cha wenzetu kumdhalilisha Spika wa Bunge pamoja na kuonyesha msimamo kwamba Wabunge Watanzania vile vile tuna msimamo na hatukubali kuyumbishwa.
Baada ya hapo, ndio tuliweza kukaa meza moja na kufikia makubaliano kwamba Arusha ipate vikao viwili na Tanzania vile vile ipate kikao kimoja. Makubaliano hayo yalipelekea Motion ya kutaka vikao vifanyike kwa mzunguko kufanyanyiwa marekebisho ili kuongeza Arusha kupata Vikao viwili na Tanzania kimoja sambamba na nchi zingine za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kupata vikao kwa njia ya mzunguko.
Vikao vya Arusha vina umuhimu sana kwani ni Kikao cha Bajeti kitasaidia kupunguza gharama kubwa kwani wafanyakazi wa Secretariet, Maafisa pamoja na vitabu vya bajeti na vitendea kazi havitasafirishwa nchi yeyote isipokuwa vitabaki Arusha. Hali kadhalika kikao cha Ukaguzi vile vile kitapunguza gharama kwa kiasi kikubwa.
Mhe. Adam Kimbisa
Mwenyekiti

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video