Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
KOCHA
wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini England, Manchester
United, David Moyes amesema yuko tayari kuivaa Liverpool leo katika
kombe la Capital One, lakini amekiri kuwa anahitaji wachezaji wapya
wawili ili kushinda mataji.
Moyes
amesema amekubali kukosolewa kwake baada ya kipigo cha jumapili ya wiki
iliyopita cha mabao 4-1 katika mechi ya watani wa jadi, Manchester
United dhidi ya Manchester City.
Lakini
kukosolewa kwa Moyes kulianza hata kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa
ligi kuu, hasa baada ya kushindwa kuwashawishi wachezaji wengi kujiunga
na United katika dirisha la majira ya kiangazi.
Kichwa chamgonga kweli: David Moyes bado amechanganyikiwa na kipigo cha 4-1 jumapili kutoka kwa wanaume wa kazi Manchester City
Klabu
ya Man United ilishindwa kumsajili Thiago Alcantara na Cesc Fabregas
kutoka FC Barcelona, wakati huo huo nyota wa Real Madrid, Mesut Ozil
aliyekuwa akiwindwa pia alijiunga na Arsenal kwa dau lililovunja rekodi
ya klabu hiyo la pauni milioni 42.5.
Alipoulizwa
kama anahitaji wachezaji zaidi, Moyes alisema: ‘Ni kweli tunahitaji
kuleta wachezaji wapya, sio kwenye kikosi moja kwa moja, lakini ni
kuangalia kwanza. Nadhani hili litatekelezwa”
“Tunaelekea
dirisha dogo la usajili, mara zote tunasema tutapambana kutafuta
wachezaji na tutatuma ofa nyingi zaidi na zaidi. Kiukweli nahitaji
kupata wachezaji wawili zaidi”.
Duuh!
kali kweli: Hofu ya Moyes inazidi kushika kasi baada ya kutunguliwa
mabao 4-1 na Manuel Pellegrini, na amekiri kuwa kipigo kama hicho
kinaweza kutokea kweli
Usajili mkubwa: Mscotishi aliungana tena na kiungo wake wa zamani akiwa Everton Marouane Fellaini katika majira ya kiangazi
na mabaya kwake
Kocha
huyo wa zamani wa Everton amekutana na wakati mgumu katika mechi ya
kwanza ya watani wa jadi ” Manchester derby”, kitu ambacho ni tofauti na
kocha mwenzake ambaye ni mpya pia Manuel Pellegrini.
City
walisajili wachezaji wengi kuliko United majira ya kiangazi, na
kuondoka kwa kocha aliyekuwa na ushawishi mkubwa, Alex Ferguson, Moyes
amesema kuwa kikosi chake kwa sasa kipo kipindi cha mpito.
Aliongeza “Tuna siku kama ya jumapili na lazima zitatokea zaidi kwa wakati huu wa mpito”
0 comments:
Post a Comment