Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho anatarajia kuongea kwa mara ya mwisho na mmiliki wa klabu, Roman Abramovich ili asajili mshambuliaji mwingine kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili kesho jumatatu.
Mpaka sasa kocha, Mourinho amewatumia washambuliaji wake, Fernando Torres, Demba Ba na Romelu Lukaku, ambao kwa pamoja walifunga mabao 12 katika mechi za maandalizi ya ligi kuu nchini England, lakini bado hajaridhishwa na uwezo wao.
Huyu bwana ana balaa: Fernando Torres (kushoto) amekuwa butu sana Chelsea
Mourinho mwishoni mwa wiki iliyopita alimsainisha mkataba wa mwaka mmoja, Samuel Eto’o kutoka Anzi, hata kama ana miaka 32, bado atamtumia Mcameroon huyo kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza.
Wawili hao walifanya kazi vizuri wakiwa Inter Milani. Ingawa muda ni mfupi, Mourinho atafurahi kumuona nyota huyo wa heshima akisimama kama namba 9 bora.
Kocha huyo mwenye jeuri kubwa ya maneno anataka kumsajili nyota wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski na Karem Benzema, ambaye alikuwa mshambuliaji wake mkubwa akiwa Real Madrid msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment