MECHI nne bila ushindi. Kama Rafa Benitez angekuwa bado yupo kazini, anerushiwa mayai viza.
Jose
Mourinho amepata kipigo katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya
Mabingwa baada ya Chelsea kuchapwa mabao 2-1 nyumbani na FC Basle.
Oscar
alitangulia kuwafungia The Blues dakika ya 45, lakini Salah
akasawazisha dakika ya 71, kabla ya Streller kufunga la ushindi dakika
ya 82 Uwanja wa Stamford Bridge.
Kikosi
cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Oscar, van
Ginkel/Mikel dk75, Lampard/Ba dk76, Willian/Mata dk67, Eto’o na Hazard.
Basle: Sommer, Voser, Schar, Ivanov, Safari, Salah/Xhaka dk88, Diaz, Frei, Stocker/Ajetidk 83, Sio/Delgado dk65 na Streller.
Mkono kichwani: Frank Lampard (kushoto) akionekana mnyonge wakati Basle wanashangilia ushindi wao Stamford Bridge
Wanyonge: Gary Cahill, Oscar na John Obi Mikel wakisikitikia kipigo
Mshindi wa mechi: Marco Streller (wa pili kushoto) akiifungia bao la ushindi Basle
Mkali wa vichwa: Streller (katikati kushoto) akishangilia na mfngaji mwenzake Mohamed Salah
Bao: Mohamed Salah (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake wa Basle baada ya kusawazisha
Huzuni tu: Jose Mourinho amefungwa mechi ya pili tangu arejee Stamford Bridge
Ujumbe kwa kocha: Shabiki la Chelsea akipeleka ujumbe kwa kocha Mourinho kwamba Juan Mata anastahili kucheza na si kukaa benchi
Wakati huo huo ARSENAL imeanza vyema Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Marseille Uwanja wa Velodrome, Ufaransa.
Mabao
ya Gunners yalifungwa na Theo Walcott dakika ya 65 na Aaron Ramsey
dakika ya 83, wakati la wenyeji lilifungwa na Jordan Ayew kwa penalti
dakika ya 90.
Kikosi
cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Gibbs, Koscienly, Mertesacker, Sagna,
Flamini/Myaichi dk90, Wilshere, Ramsey, Ozil, Walcott/Monreal dk77 na
Giroud.
Marseille:
Mandanda, Fanni, N’Koulou, Mendes, Morel, Romao, Imbula/Thauvin dk79,
Payet/J.Ayew dk72, Valbuena/Khalifa dk89, A. Ayew na Gignac.
Kitu hicho: Theo Walcott ameifungia Arsenal
Kitu kingine: Aaron Ramsey amefunga bao la sita msimu huu
Si mchezo wangu: Mesut Ozil alicheza kiungwana katika ukabaji wake
Kipaji: Theo Walcott akipambana na kiungo wa Marseille, Mathieu Valbuena
0 comments:
Post a Comment