Sunday, September 1, 2013


Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, “Taifa kubwa” kesho wanatarajiwa kushuka dimbani katika mchezo wa kirafiki uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na Mafunzo ya Zanzibar, huku mechi hiyo ikiwa na faida ya kujiandaa na mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mtibwa septemba 14 mwaka.
Simba walianza ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 kwa mechi mbili za ugenini, ambapo mechi ya ufunguzi walitoka sare ya 2-2 na Rhino Rangers ya Tabora katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, na mechi ya pili walishinda bao 1-0 dhidi ya JKT Oljoro katika uwanja wa Sheikh Amri Kaluta Abeid jijini Arusha.
Afisa habari wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga amesema mara baada ya safari ya mikoa ya Tabora na Arusha kwenye mechi mbili za awali za Ligi Kuu ya Tanzania, timu ya Simba imerejea salama jijini Dar es Salaam ikiwa na kikosi chake kamili tayari kujiandaa na mechi ijayo ya ligi kuu.
“Kama sehemu ya maandalizi ya mechi hiyo, kikosi cha Simba kitashuka dimbani katika Uwanja Mkuu wa Taifa siku ya kesho, Jumatatu Septemba 2, kucheza na Mafunzo ya Zanzibar katika mechi ambayo ina faida nyingine zaidi ya kuwa ya kujiandaa na mechi ya Mtibwa”. Alisema Kamwaga katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo.
HenryJoseph
Kamwaga ametaja  faida za mechi hiyo, Mosi, mechi hiyo itatoa nafasi kwa wapenzi na wanachama wa Simba, pamoja na washabiki wa soka kwa ujumla wake, kupata fursa ya kuwaona kwa mara ya kwanza wachezaji wapya watatu wa klabu ambao hawajawahi kuonekana wakicheza jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao ni Henry Joseph Shindika aliyetoka Kongsvinger ya Norway, Gilbert Kaze na Amissi Tambwe waliotoka katika klabu ya Vital’o ya Burundi. Ingawa hawa ni wachezaji wa Simba lakini hawakutambulishwa katika Tamasha la Simba Day kama ilivyo ada kwa wachezaji wote wapya.
Mechi ya Mafunzo itatoa fursa hiyo ya kutambulishwa na kuonekana wakiitumikia klabu kwa mara ya kwanza jijini hapa.
Pili, Kamwaga amesema mechi hiyo itatumika na klabu kwa ajili ya mchezaji wake, Kiggi Makassi, ambaye atawaaga washabiki rasmi kwa ajili ya safari yake ya kwenda nchini India anakokwenda kwa matibabu ya goti lake. Kiggi anatarajiwa kuondoka jijini Septemba tisa mwaka huu.
Kwa vile Septemba 2 inaangukia siku ya kazi, waandaaji wa pambano hilo wamepanga ianze saa 11 jioni ili kutoa nafasi kwa wapenzi wengi zaidi kuhudhuria pambano hilo.
simba3Kifaa kipya cha simba Gilbert Kaze kutoka Burundi kutambulishwa kesho katika mechi maalumu dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar (Picha na Mzuka wa Fungo)
simba4Nyota mpya wa kufumania mabao kutoka Burundi na mfungaji bora wa michuano ya Kagame mwaka huu, Amissi Tambwa kesho kutambuliswa mbele ya mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba (Picha na Mzuka wa Fungo)
VIINGILIO
KATIKA pambano hilo viingilio vitakuwa ni Sh 20,000 kwa VIP A, Sh 10,000 kwa VIP B, Sh 8,000 kwa VIP C na Sh 5,000 kwa mzunguko.
Maandalizi yote kwa ajili ya mechi yamekamilika na timu zote tayari ziko jijini Dar es Salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video