Thursday, September 5, 2013

10Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba  wanatarajia kushuka dimbani katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika kesho Ijumaa, Septemba 6 mwaka huu dhidi ya mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya visiwani Zanzibar, KMKM, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Afisa habari wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga inafafanua kuwa lengo kuu la mechi hiyo ni mazoezi ya klabu hiyo kujiandaa na mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mtibwa Sugar,  Septemba 14 mwaka huu uwanja wa Taifa. 
“Kikosi kamili cha KMKM kimewasili mjini Dar es Salaam tayari na leo saa tano na nusu kamili nahodha wake, Abdi Kassim Babi na kocha mkuu wa timu hiyo wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika mgahawa wa City Lounge katikati ya jiji”. Alisema Kamwaga.
Kamwaga ameongeza kuwa Simba inaendelea na mazoezi yake jijini Dar es salaam na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya mechi hiyo.
Afisa habari huyo alifafanua kuwa mechi hiyo itaanza majira ya saa 11 jioni ili kuwezesha watu wengi kwenda uwanjani kutazama mechi hiyo ikizingatiwa kuwa Ijumaa ni siku ya kazi.
Mechi hiyo inakuja muda mfupi baada ya kufanyika mechi maalumu septemba 2 mwaka huu ya kuwatambulisha nyota wake wapya, Henry Joseph, Gilbert Kaze na Amisi Tambwe dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 4-3 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wakati huo huo Kamwaga ameeleza kuwa:  Kufuatia tangazo la Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, kuhusu Mkutano wa Katiba uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu, klabu imeanzisha rasmi mchakato wa kuwa na Katiba Mpya itakayokwenda na wakati.
Kutokana na umuhimu wa mawazo ya Wana Simba ndani na nje ya nchi kufahamika kupitia mchakato huu, klabu imeanzisha email maalumu iitwayo [email protected]  ambapo wana Simba na wapenzi wa soka kwa ujumla wanatarajiwa kuwasilisha mawazo na michango yao kuhusu nini kinapaswa kuingizwa katika Katiba mpya ya klabu.
Uongozi wa Simba unawaomba wapenzi na washabiki wa soka popote walipo duniani kuchangia mawazo katika njia hii. Mawazo yatakayochangiwa kwenye email hii yatatumika katika kutengeneza rasimu ya Katiba hiyo na rasimu hiyo itapelekwa kwenye matawi yote ya klabu kwa ajili ya kujadiliwa na wanachama.
Mawazo hayo ya wanachama yatasaidia katika kutengeneza Katiba ambayo hatimaye itawasilishwa kwenye Mkutano wa Novemba kwa ajili ya mapitio na kupitishwa.
Wana Simba wanatakiwa kujitokeza katika mchakato huu kwa faida ya kujenga Simba ya kisasa na yenye tija na ufanisi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video