Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akipokewa na Founder, Benefactor and Chief Executive
Officer wa Taasisi ya Opportunity Education Bwana Joe Ricketts kwenye
uwanja wa ndege katika mji wa Omaha uliopo katika Jimbo la Nebraska
nchini Marekani tarehe 27.9.2013
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Kate Stephens,
7, mara baada ya Mama Salma kutua kwenye uwanja wa ndege wa Omaha huko
Nebraska nchiniMarekani tarehe 27.9.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akionyeshwa na Bwana James Ricketts,
President and Chief Operations Officer, wa Taasisi ya Oppoturnity
Education shughuli mbalimbali za kununua na kusafirisha vifaa vya elimu
kwenda kwenye shule katika nchi mbalimbali hapa duniani ikiwamo Tanzania
wakati Mama Salma alipotembelea Taasisi hiyo yenye Makao Makuu yake
huko Omaha katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani tarehe 27.9..2013. Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea
zawadi ya ngao kutoka kwa Bwana Joe Ricketts, Founder, Benefactor and
Chief Executive Officer wa Taasisi ya Opportunity Education iliyoko huko
Omaha nchini Marekani. Bwana Ricketts alitoa zawadi hiyo kwa kutambua
mchango mkubwa sana alioufanya Mama Salma binafsi na Taasisi yake ya
WAMA Foundation katika masuala ya elimu. Afya na uwezeshaji kwa akina
mama..
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo
na uongozi wa juu wa Taasisi ya Opportunies Education kwenye ofisi za
taasisi hiyo huko Omaha Nebraska nchini Marekani tarehe 27.9.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwenye Mji Mkuu wa Jimbo la
Nebraska, Lincoln, huko Marekani na Dr. Natalie Hahn, Mwanzilishi wa
Malaika Foundation na Senior Private Adviser for the United Nations Fund
for International Partnership (UNFIP) tarehe 27.9.2013. Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Dr. Marjorie Kastelnik, Dean,
College of Education and Human Sciences kwenye Chuo Kikuu cha Nebraska
ambapo Mama Salma alishiriki kwenye Gala to support Global Education
kwenye Chuo Kikuu cha Lincoln huko Nebraska tarehe 27.9.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Bwana Joe Ricketts kwenye gala to support Global Education .
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia waalikwa waliohudhuria Gala to
support Global Education iliyoandaliwa kwa ajili ya kumtunuku tuzo
maalum Bwana Joe Ricketts kwa juhudi zake za kuboresha elimu duniani
hasa katika nchi zinazoendelea.
PICHA NA JOHN LUKUWI
0 comments:
Post a Comment