Friday, September 6, 2013


Pix 1Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
RAIS wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa amesema mafanikio ya utoaji wa huduma za  afya  nchini yatafikiwa  kutokana na moyo wa kujituma, ushirikiano uliopo kati ya wafanyakazi, Serikali na taasisi za kifedha ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika sekta  hiyo.
 Rais huyo ambaye  pia  ni  mwasisi wa taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na masuala ya Afya ya Benjamin William Mkapa (The Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF) alisema hayo katika hafla ya uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka mitano (2013-2018) wakati wa  hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Aliongeza kuwa ubora wa utoaji huduma za afya unaongozwa na misingi ya ubunifu, hekima, upendo na moyo wa kushirikiana.
“Mpango mkakati huu tunaozindua unasisitiza maeneo makuu matano inayojishughulisha na masuala ya ukimwi (HIV/AIDS) ambayo yanaenda sanjari na hali ya afya, ushahidi unaosimamia suluhisho la afya ya rasilimali watu,”alisema Rais mstaafu Mkapa.
Mkapa aliongeza kuwa mpango mkakati huo unalenga kuwajengea uwezo bora wa taarifa za kiutawala, elimu na mawasiliano (Education and Communication (IEC), mifumo ya uendeshaji bora wa biashara endelevu na uwezo wa utawala katika masuala ya kitaalamu.
Katika kipindi hicho, BMAF itaendelea kuratibu na kusimamia taasisi mbalimbali ambazo ni za kiserikali na zisizo za kiserlikali (NGO’s), makampuni na taasisi binafsi, taasisi za kidini na   asasi za kijamii (CBO’s).
Alisema Mfumo wa utoaji huduma zinazotolewa unazingatia malengo ya taasisi hiyo na kufuatilia na kutekeleza maamuzi ya serikali katika kuimarisha utoaji huduma za afya nchini.
Aidha mfumo huo una lengo la kuimarisha utoaji bora wa huduma za afya, ili ziweze kufikia umma wote wa Watanzania hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya BMAF Meja Jenerali (Rtd) Herman Lupogo alisema kuwa mpango mkakati huo umetoa unabainisha malengo yanayotarajiwa kufikiwa ndani ya miaka mitano, ikiwa na mantiki ya kuboresha utoaji wa huduma za afya hasa kwa makundi maalimu ya wanawake, wanaume, vijana na watoto nchini.
Taasisi  hiyo  ilianzishwa mwaka 2006 baada ya kukamilisha hatua zake za msingi za awali na – the Mkapa Fellows Programme.
Taasisi ya BMAF ilianzishwa mwaka 2006 baada ya kukamilisha hatua zake za msingi za awali na washirika wa mpango huo( Mkapa Fellows Programme).
Ushirika huo  ulianzishwa mwaka 2005 kwa juhudi  za pamoja kati ya Rais  huyo  na Rais wa 41 wa Marekani William Jefferson Clinton.
Taasisi hizi rafiki zilikuwa ni mwanzo wa malengo imara, ubunifu unaosimamiwa na BMAF kwa lengo la kusimamia masuala ya afya ya jamii nchini.
Wadhamini wa wakuu katika tamasha la chakula cha jioni walikuwa Banki- M (M- Corporate and Investment Foundation Bank), Shirika la Bima ya Afya la Taifa (NHIF), Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Serena Hotel. Hafla hiyo iliandaliwa taasisi hiyo na kusimamiwa na kampuni ya Montage

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video