Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ametaka kuzidishwe mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la ash-Shabab.
Nicholas
Kay ameyasema hayo leo katika kikao na waandishi wa habari mjini
Geneva, Uswis na kuitaka jamii ya kimataifa izidishe juhudi za kupambana
na kundi hilo. Amesema kuwa hadi sasa serikali ya Somalia imeweza kwa
kiasi fulani kurejesha hali ya usalama katika maeneo mengi ya nchi hiyo
na akaongeza kuwa, pamoja na hayo bado kuna haja ya kuisaidia nchi hiyo
kwani serikali ya Mogadishu bado inakabiliwa na kundi hilo.
Kay
amesema shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa al Shabab dhidi ya
jengo la kibiashara huko mjini Nairobi, Kenya sio la kushangaza, kwani
ni miongoni mwa jinai kubwa ambazo zimekuwa zikitekelezwa na kundi hilo.
Amesema kuwa, usalama wa Somalia unategemea kusambaratisha kwa kundi
hilo la ash-Shabab.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon ameiomba jamii ya
kimataifa kusaidia juhudi za kuliangamiza kundi la kigaidi la al Shabab
ambalo limetangaza kwua ndilo lililotekeleza shambulizi dhidi ya jumba
la maduka la Westgate jijini Nairobi.
CHANZO: RADIO TEHRAN
0 comments:
Post a Comment