Miss
Utalii Tanzania 2013, Hadija Mswaga, anaondoka nchini siku ya Jumanne
Tarehe 1-10-2013 kuelekea Equatorial Guinea kuwakilisha Tanzania katika
Mashindano ya Dunia ya Miss Tourism World 2013. Atasafiri kwa ndege ya
shirika la ndege la Ethiopian Airline.
Katika
mshindano hayo yanayoshirikisha nchi 126 duniani kote, na kuoneshwa
LIVE katika Televisheni Duniani kote, Miss Utalii Tanzania 2013, anabeba
ujumbe wa kutangaza Hifadhi ya Ngorongoro Crater kama moja ya maajabu
ya Dunia Afrika.
Akitoa
sababu za kuibeba Hifadhi ya ngorongoro katika mashindano hayo, Hadija
Mswaga, alisema kuwa mbali ya hifadhi hiyo kuwa ni ya kipekee duniani,
lakini ndiyo hifadhi ambayo chimbuko la binadamu wa kwanza kuishi
duniani, pia hifadhi hiyo ndio kitovu cha hifadhi ya faru nchini, mbali
ya kuwa ndiyo hifadhi pekee duniani ambako binadamu na wanyama wanaishi
na kushirikiana maisha ya kila siku bila ya kudhuriana.
Wakati
sasa umefika tena wakati sahihi kwa hifadhi ya ngorongoro kuwa hifadhi
kiongozi kwa umaarufu ,pato la utalii na kutembelewa na watalii wengi
zaidi duniani alisema hadija.
0 comments:
Post a Comment