Huku
hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate
lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye
maduka na mikahawa zaidi ya themanini.
Wapiganaji
wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani.
Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi
mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua
risasi kiholela.
Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Helikopta
za polisi zinapaa juu ya jengo hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika
doria. Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru
waathiriwa wakati hali ikiwa ni ya ati ati katika eneo la shambulizi.
Awali
jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado
limetaja hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka
waliosalia ndani ya jengo hilo.
Ripoti
zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab
kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa. Baadhi wametibiwa na kuondoka
hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na
kutokana na guruneti ambalo Al shabaa waliwarushia wale waliokuwa ndani
ya mikahawa siku ya Jumamosi.
Kundi
hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya kenya
kupelekeka majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji
hao.
CHANZO: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment