Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) Mhe. William V.
Lukuvi (MB) kuanza ziara rasmi leo tarehe 16 hadi 19 Septemba, 2013
katika Mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya.
Katika
ziara hiyo Waziri Lukuvi anatarajiwa kutembelea baadhi ya vituo vya
Ununuzi wa Mahindi kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye Maghala ya National
Food Reserve Agency (NFRA), Maghala ya NFRA ya kuhifadhi chakula,
atapokea taarifa ya Utekelezaji kuhusu Mradi wa Miundo Mbinu ya Masoko
na Uongezaji wa Thamani (MIVARF) katika maeneo yanayotekeleza mradi huu.
Vilevile
Mhe. Lukuvi atapokea Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi yote ya Maendeleo
ikiwemo Miradi itokanayo na ahadi za Mhe. Rais na Miradi itokanayo na
Ilani ya Chama Tawala pamoja na Miradi inayofadhiliwa na Taasisi
mbalimbali Mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment