Mhe.Ummy
Mwalimu akipata maelezo ya namna vyakula mbalimbali vinavyosindikwa
kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Upendo Development Bibi.Lydia Jacob
alipokitembelea kikundi hicho Mhe.Ummy
Mwalimu akipokelewa na Kikundi cha Vicoba cha Kinana cha Tupendane
alipowatembelea kuona namna kikundi hicho kinavyoshiriki katika shughuli
za kujiinua Kiuchumi
Naibu
Waziri Maendeleo ya Jamii,Mhe.Ummy Mwalimu akisalimiana na Wanafunzi
wanaosoma Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kisarawe alipowatembelea Chuoni
hapo,Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Bw. Isaya Mwambogela
Katika
Picha ni Pamoja na Mhe.Ummy Mwalimu Naibu Waziri,MKuu wa Wilaya ya
Kisarawe Mhe. Fatma Kimario na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto
Wilayani hapo
…………..
Mhe.
Naibu Waziri ameendelea na ziara yake Wilayani Kisarawe, ambapo katika
kufuatilia utekelezaji wa Sera na program mbalimbali za Wizara ikiwemo
masuala yanayohusu Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wanawake, Watoto na
ufuatiliaji wa shughuli za NGOs, Mhe amepata nafasi ya kukutana na
Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto ya Wilaya ametembelea vikundi vya
uzalishaji vya wanawake ambavyo vinawawezesha kujiinua kiuchumi,
vilevile ametembelea Chuo cha Maendeleo ya Wananchi cha Kisarawe.
Aidha,
katika ziara yake Wilayani humo, Mhe. Ummy amesisitiza umuhimu wa
watoto kupewa ulinzi wa kutosha ili kuwaepusha na vitendo vya Kikatili
na vilevile ameitaka Halmashauri hiyo,kuhakikisha kuwa,wanafunzi wote
waliomaliza darasa la saba hivi karibuni Wilayani humo hawaolewi kabla
na baada ya matokeo yao kutoka, badala yake wawahamasishe wananchi
kuwaendeleza watoto wao kielimu.
0 comments:
Post a Comment