Pichani: Mheshimiwa Dk. Migiro akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa
Ubalozi. Kutoka kushoto ni Amos Msanjila, Allen Kuzilwa, Rose Henry
Kiondo, Wema Kibona, Idris Zahran, Caroline Kitana Chipeta na Yusuf
Kashangwa.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) na Katibu wa NEC wa Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa
Dk. Asha-Rose Migiro atembelea Ubalozi wa Tanzania hapa London, kwa
lengo la kuwasabahi maafisa wa Ubalozi na kuwapatia taarifa mbalimbali
za maendeleo ya ushiirikiano na vyama marafiki na CCM, hususan Chama cha
Labour cha Uingereza.
Mhe.
Dk. Migiro alipita Ubalozini akitokea mji wa Brighton, Kusini mwa
Uingereza alikokuwa akihudhuria Mkutano Mkuu wa wa Chama cha Labour
uliofanyika huko kuanzia tarehe 22 hadi 25 Septemba 2013. Katika
mazungumzo yake na maafisa hao Dk. Migiro aliwadokeza kuwa akiwa
Brighton alifanikiwa kukutana na kuanzisha mawasiliano na maafisa
mbalimbali wa Chama cha Labour kwa lengo la kuimarisha zaidi ushirikiano
wa vyama vyao.
0 comments:
Post a Comment