WAKATI
muda unazidi kuyoyoma kuelekea mchezo mkali wa ligi kuu soka Tanzania
bara hapa jijini Mbeya baina ya wenyeji wa uwanja wa sokoine,
“Wajelajela”, Tanzania Prisons dhidi ya wakali wa mashamba ya miwa ya
Manungu Turiani Mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar, kocha wa klabu ya Mtibwa,
Mecky Mexime ametoa kali ya mwaka baada ya kuwaponda vikali wanaosema
uwanja huu ni mbovu.
Akizungumza
jijini hapa, Mexime amesema wanaosema uwanja wa Sokoine na mbaya hawana
maana yoyote katika soka la Tanzania, kwani umekaguliwa na TFF na
umekubalika, zaidi hata hao wanaosema uwanja haufai, hawana hata wa
mazoezi.
“Mbona
viwanja vyetu tunavijua sana, hawa wanaosema uwanja huu ni mbovu, mbona
wanafanyia mazoezi viwanja vibovu zaidi. Waache siasa katika soka pale
wanaposhindwa, wacheze mpira na kuacha visingizio visivyokuwa ba
maana”. Alisema Mexime.
Zaidi
Mexime amewaacha hoi mashabiki wa soka baada ya kusema kuwa; kama mtu
anasema uwanja wa Sokoine mbaya, anataka mpira ukachezwe kwenye magodoro
ya vitandani?.
“Kama uwanja huu ni mbaya, sasa wanataka tukachezee kwenye magodoro?”. Alihoji Mexime.
Akizungumzia
pambano la leo dhidi ya Tanzania Prisons, Mexime amesema itakuwa mechi
nzuri sana na yenye mvuto kwani daima klabu yake inacheza soka la
kuvutia.
“Sisi kazi yetu ni kucheza soka, sio kama hao wanaosingizia uwanja kila kukicha, tutapiga soka la ukweli”. Alisema Mexime.
Wakati huo huo nao Tanzania Prisons wamesema wako makini na mechi ya leo, hivyo wamewatoa shaka mashabiki wa Mbeya.
Kocha
mkuu wa klabu hiyo, Jumanne Chale amesema wachezaji wake wana morali
kubwa ya kusaka ushindi na kwa kiasi kikubwa wanategemea kushinda baada
ya kutoa sare jumatano ya wiki hii dhidi ya Yanga.
Wao Mtibwa walitoa suluhu na Mbeya City katika uwanja wao wa Manungu siku ya jumatano.
0 comments:
Post a Comment