AMEJIBU;
Lionel Messi amejibu mapigo ya mpinzani wake, Cristiano Ronaldo wa Real
Madrid baada ya kuifungia hat-trick Barcelona katika ushindi wa 4-0
dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa
Nou Camp.
Muargentina huyo pamoja na kufunga mabao matatu peke yake usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique.
Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson.
Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdes, Alves, Pique/Bartra dk80, Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas/Xavi dk72, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar /Pedro dk72.
Ajax: Vermeer, van Rhijn, Denswil, Moisander/van der Hoorn dk73, Blind/Schone dk78, Poulsen, de Jong/Serero dk59, Duarte, Bojan, Sigthorsson na Boilesen.
Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdes, Alves, Pique/Bartra dk80, Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas/Xavi dk72, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar /Pedro dk72.
Ajax: Vermeer, van Rhijn, Denswil, Moisander/van der Hoorn dk73, Blind/Schone dk78, Poulsen, de Jong/Serero dk59, Duarte, Bojan, Sigthorsson na Boilesen.
Mkwaju: Messi alifunga bao la kwanza kwa shuti la mbali la mpira wa adhabu
La pili: Messi akifunga bao lake la pili
Kiulaini: Messi akimtoka beki Stefano Denswil
Tabasamu: Messi akishangilia na beki wake, Dani Alves
Sergio Busquets akidhibiti mpira katikati ya wachezaji wa Ajax, Siem de Jong (kushoto) na Lerin Duarte
Anakosa: Kolbeinn Sigthorsson alikosa penalti iliyochezwa na kipa Victor Valdes
Alexis Sanchez akimvaa Daley Blind wa Ajax Uwanja wa the Camp Nou
Beki wa Barcelona, Adriano akimdhibiti Ricardo van Rhijn wa Ajax
Pique akienda hewani kuifungia Barcelona bao la tatu
Wako vizuri: Barca wakishangilia ushindi wao Camp Nou
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, AC Milan iliichapa Celtic 2-0 Uwanja wa San Siro, mabao ya Zapata dakika ya 82 na Muntari dakika ya 85.
Kikosi
cha AC Milan kilikuwa: Abbiati, Zaccardo, Zapata, Mexes,
Constant/Robinho dk76, Nocerino, De Jong, Muntari, Birsa/Emanuelson
dk64, Matri/Poli dk87 na Balotelli.
Celtic:
Forster, Lustig, Van Dijk, Ambrose, Izaguirre, Matthews/Boerrigter
dk75, Brown, Mulgrew/Biton dk89, Samaras, Commons/Pukki dk77 na Stokes.
Christian Zapata akitimka kushangilia baada ya kuifungia bao la kwanza AC Milan dhidi ya Celtic
Mwafrika hatari: Sulley Muntari wa Milan akishangilia baada ya kufunga bao la pili zikiwa zimebaki dakika tano
Phillipe Mexes akimrukia Cristian Zapata baada ya Mcolombia kufunga
Ukuta mgumu: Wachezaji wa AC Milan wakiwa wameweka ukutawakati beki wa kati wa Celtic, Charlie Mulgrew akipiga mpira wa adhabu
0 comments:
Post a Comment